Wednesday, January 02, 2013

IRAN YAJARIBU MAKOMBORA YAKE MAPYA


Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanyia majaribio makombora mawili ya Qader (Uwezo) ya pwani kwa bahari na Nour (Nuru) ya juu kwa juu katika mazoezi ya kijeshi ya 'Velayat 91'.
Akizungumza na waandishi habri, Admeli Ali  Vafadar Kamanda wa Kitengo cha Makombora cha Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema makombora hayo mawili yalitengenezwa hapa nchini na wataalamu Wairani. Ameongeza kuwa makombora hayo yameimarisha kiwango cha uwezo wa Jeshi la Wanamaji la Iran baharini. Maneva hayo ya siku sita yalianza Ijumaa, tarehe 28 Disemba, na yanafanyika katika eneo pana la fukweni, baharini na angani kwenye lango la Hormuz, Bahari ya Oman, kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden na lango la Babul Mandab.
Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari amesema maneva hayo ya kijeshi ya Iran yana ujumbe wa urafiki na udugu kwa mataifa rafiki na onyo kali kwa maadui.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO