Sunday, July 28, 2013

ALIYEFUTWA KAZI SUDAN KUWANIA URAISI SUDAN

Aliyekuwa makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar amesema atagombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 dhidi ya Rais Salva Kiir aliyemfuta kazi mapema wiki hii. Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana kwa mara ya kwanza tangu kufutwa kazi, Machar alisema atawania kupitia chama tawala na kumpinga Kiir. Machar ameongeza kuwa ili taifa hilo liungane haliwezi kuvumilia utawala wa kiimla.Rais Kiir alivunjilia mbali baraza la mawaziri na kumfuta kazi makamu wake siku ya Jumanne kufuatia ripoti kuwa kuna mzozo wa uongozi ndani ya chama tawala hasa kati ya Kiir na Machar.Kiir amepunguza idadi ya mawaziri kutoka 29 hadi 18. Pia alimsimamisha kazi katibu mkuu wa chama cha SPLM Pagan Amum akisubiri kukamilika kwa uchunguzi wa madai ya kudharau mamlaka na kuleta mgawanyiko ndani ya chama tawala. Machar amesema Kiir ana haki kikatiba kumfuta kazi makamu wa rais na kulivunja baraza la mawaziri lakini amemshutumu kwa kile alichokiita pengo la uongozi lilioachwa baada ya hatua hiyo kwa kushindwa kujaza nafasi zao mara moja.

MAZUNGUMZO KATI YA ISRAEL NA PALESTINA KUANZA JUMANNE

Wapatanishi wa Israel na Palestina watakutana mjini Washington Marekani Jumanne ijayo kufufua  mazungumzo ambayo yalikuwa yamekwama kwa miaka mitatu. Afisa mmoja wa wapalestina ambaye hakutaka jina lake kutajwa ameliambia shrika la habari la Afp kuwa ujumbe wa Palestina utaongozwa na  Saeb Erakat huku ule wa Israel ukiongozwa na waziri wa sheria Tzipi Livni na kuongeza kuwa maafisa wa Marekani pia watashiriki. Waziri wa maendeleo ya kanda wa Israel Silvan Shalom mapema wiki hii alisema mazungumzo hayo yataanza Jumanne lakini haikuwa imethibitishwa tarehe hiyo wala mahali watakapokutana. Mjumbe mkuu wa Israel Livni ataandamana na balozi wa kibinafsi wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Yitzhak Molcho.Kulingana  na maafisa wakuu wa Israel agenda kuu ya mkutano huo wa washington itakuwa juu ya jinsi ya kufanya mazungumzo hayo na pia  mada zitakazojadiliwa pamoja na ratiba yake.Kituo cha redio nchini humo kimesema leo wafungwa zaidi ya 100 wanatarajiwa kuachiliwa huru katika kipindi cha mazungumzo hayo ambayo yanatarajiwa kudumu kwa kati ya miezi sita na tisa.

MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA UJERUMANI

Maelfu ya watu wameandamana nchini Ujerumani kupinga mpango wa udukuzi wa Marekani. Waandamanaji hao wameitikia wito wa kundi linalojiita stopwatching us na kuvumilia joto na jua kali kuandamana katika miji ya Hamburg,Munich,Berlin na miji mingine 35 nchini humu.Baadhi ya waandamanaji hao walivaa kofia kubwa kuzuia jua huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kutaka kukomeshwa kufuatiliwa kwa data za simu na mitandao.Huku hayo yakijiri,raia wengi nchini humu wamemiminika katika vidimbwi vya maji,maziwani na fuoni kupunguza makali ya joto ambalo limekuwa likiongezeka katika msimu huu wa kiangazi na kufikia nyuzi 39 za celisius.Wataalam wa utabiri wa hali ya hewa wamesema Ujerumani huenda  itarekodi kiwango cha juu zaidi cha nyuzi 40.2 hapo kesho ambacho mara ya mwisho kilishuhudiwa mwaka 1983.Mvua ya ngurumo wikendi hii inatarajiwa kuleta afueni kwa kiasi fulani kabla ya viwango vya joto kupanda tena wiki ijayo.   

WAPINZANI SYRIA WATAKA ASSAD KUSHINIKIZWA MABADILIKO

Muungano Mkuu wa wapinzani nchini Syria umeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kumshinikiza Rais Bashar al-Assad kukubali kuingia katika makubaliano ya kumaliza machafuko ya kisiasa yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili wakati wa utawala wake. Mkuu mpya wa Muungano huo Ahmad Jarba ameliambia baraza la usalama kuwa shinikizo zaidi toka jumuiya ya kimataifa linahitajika ili serikali ya Assad ikubali kwenda sambamba na mabadiliko ya kisiasa. Aidha wapinzani hao wametaka jumuiya ya kimataifa kuishinikiza Urusi kusitisha msaada wa silaha kwa serikali ya Assad.
Wapinzani wa Rais Assad wapo katika ziara ya kuweka bayana malengo yao juu ya mgogoro wa Syria sambamba na kuomba msaada wa silaha kwa mataifa ya Magharibi. Hata hivyo mkutano wa kwanza kati ya Muungano wa wapinzani wa Syria na wanachama 15 wa baraza la usalama la umoja wa mataifa haujaonyesha dalili za mafanikio ya kusaka suluhu ya mgogoro huo ambao kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa UN umesababisha mauaji ya watu zaidi ya laki moja toka yalipoanza mwanzoni mwa mwaka 2011.

MAREKANI YASEMA HAITAMHUKUMU KIFO SNOWDERN

Serikali ya Marekani imetangaza kwamba, iwapo Russia itamkabidhi Edward Snowden kwa serikali ya Washington, haitamuhukumu adhabu ya kifo, kwa tuhuma za kufichua siri na nyaraka za Shirika la  Usalama wa Taifa la Marekani NSA. Eric Holder Mwanasheria Mkuu wa Marekani amemuandikia barua Alexander Vladimirovich Konovalov Waziri wa Sheria wa Russia na kumuhakikisha kwamba, Snowden hatateswa wala hatakabiliwa na adhabu ya kifo. Kwa muda wa wiki kadhaa sasa Snowden yuko kiwanja cha ndege cha Moscow, lakini wiki iliyopita aliomba hifadhi ya muda ya ukimbizi nchini Russia.
Edward Snowden afisa wa zamani wa shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA alifichua kwamba Washington imekuwa ikifanya ujasusi wa kimataifa kwa kudukua baruapepe za wote duniani pamoja na kusikiliza mazungumzo  ya simu kwa siri, jambo lililaaniwa na nchi mbalimbali duniani. Wakati huohuo, Baraza la Seneti la Marekani limetangaza kuwa, iwapo serikali ya Russia itampatia hifadhi ya ukimbizi Edward Snowden, kuna uwezekano kwa nchi hiyo kukabiliwa na vikwazo vya kibiashara kutoka Washington.

WAFUASI WA MORSI KUENDELEZA MAANDAMANO

Muungano unaoundwa na vyama vinavyoiunga mkono harakati ya Ikhwaanul Muslimiin nchini Misri umeahidi kuendeleza maandamano leo na kesho nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, muungano huo umesisitiza kuendelezwa  maandamano ya kipinga hatua ya jeshi la nchi hiyo ya kumuondoa madarakani Rais Muhammad Morsi wa nchi hiyo. Waandamanji hao wataka Muhammad Morsi arejeshwe kwenye wadhifa wake wa rais wa nchi hiyo.
Hapo jana, mamilioni ya waungaji mkono wa Morsi walifanya maandamano kwenye miji mbalimbali nchini humo wakitangaza uungaji mkono wao kwa rais aliyechaguliwa kwa njia za kidemokrasia. Waandamanaji hao wanamtaka AbdulFattah as Sisi mkuu wa majeshi ya Misri ajiuzulu, kwa vile alitoa amri kinyume cha sheria ya kuenguliwa Morsi madarakani. Maandamano ya jana Ijumaa ya waungaji mkono na wapinzani wa Morsi yalisababisha watu watano kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mji wa Alexandria.

120 WAUAWA MISRI KATIKA MACHAFUKO

Watu wasiopungua 120 wameuawa na wengine zaidi ya 1500 kujeruhiwa katika mapigano yaliyojiri katika miji mbalimbali kati ya wafuasi na wapinzani wa Muhammad Morsi rais wa Misri aliyepinduliwa na jeshi la nchi hiyo.Mapigano hayo yalizuka jana baada ya wafuasi wa Morsi waliokuwa wamekusanyika katika wilaya ya al Nasr huko Cairo kudai kurejeshwa madarakani rais huyo. Aidha maandamano mengine yalifanyika hiyo jana kufuatia wito uliotolewa na harakati ya Ikhwanul Muslimin ya kufanya maandamano ya amani kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani Rais Muhammad Morsi. Wakati huo huo habari zimeeleza kuwa  jeshi la Misri limekuwa likitumia silaha hai kwa wafanya maandamano   nchini humo. 

SUDAN YATAKA MSAAADA KUHUSU WAASI

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Sudan katika Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa iyalazimishe makundi ya waasi ya Darfur kukaa katika meza moja ya mazungumzo na serikali ya Khartoum. Daffa Allah Alial-Haj ameitaka jamii ya kimataifa iisaidie nchi yake katika mchakato wa kurejesha amani na utulivu katika jimbo la Darfur. Amesema, ili kufikia lengo hilo, jamii ya kimataifa inapaswa kuyalazimisha makundi ya waasi yasitishe vitendo vya utumiaji mabavu na kukaa katika meza moja ya mazungumzo na serikali ya Sudan. Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Sudan katika Umoja wa Mataifa amesema, serikali ya Khartoum inaendelea na juhudi zake za kuyakalisha katika meza moja ya mazungumzo makundi ya waasi lakini jamii ya kimataifa inapaswa kuisaidia nchi yake katika hilo. Jimbo la Dafur lililoko magharibi mwa Sudan limekuwa likikabiliwa na hali ya mchafukoge tangu mwaka 2003.

HIZBULLAH YACHELEA UGAIDI NCHI ZA KIISLAM

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imesema kuwa, ina wasi wasi juu ya kuenea ugaidi katika nchi za Kiislamu.  Sayyid Ibrahim al-Amin, Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah ya Lebanon ametahadharisha kwamba, tishio la ugaidi Palestina, Lebanon, Iraq, Libya, Syria na Misri linatia wasi wasi na hadi sasa watu wengi wameuawa na wengine kubaki bila makazi kutokana na vitendo vya ugaidi katika nchi hizo. Afisa huyo mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria jinai za Wazayuni huko Palestina na vitendo vya kinyama vinavyofanywa na magaidi huko Syria na kuhoji kwamba, kwa nini madola yanayodai kuwa vinara wa kutetea haki za binadamu ulimwenguni yamenyamazia kimya mauaji haya? Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah ya Lebanon amesema bayana kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel ndio adui mkuu wa Lebanon na muqawama wa wananchi.

SHAMBULIZI LA MAREKANI LAUA 60 AFGHANISTAN

Watu wasiopungua 60 wameuliwa katika mashambulio tofauti ya anga yaliyofanywa na vikosi vya majeshi ya kigeni yanayoongozwa na Marekani katika mikoa ya Paktia, Kunar na Helmand nchini Afghanistan. Watu wasiopungua 45 waliuliwa hapo jana wakati majeshi ya kigeni yalipofanya mashambulio ya anga katika mkoa wa Helmand ulioko kusini mwa Afghanistan. Majeshi hayo yanayoongozwa na Marekani yamezidisha mashambulio ya anga katika maeneo ya raia nchini Afghanistan katika miezi ya hivi karibuni. Vifo vya raia vinavyotokana na mashambulio ya anga yakiwemo ya ndege zisizo na rubani za Marekani vimekuwa chanzo cha misuguano kati ya serikali ya Afghanistan na vikosi vya majeshi ya kigeni yanayoongozwa na Marekani na kuzidisha pia chuki dhidi ya Washington nchini Afghanistan. Marekani na waitifaki wake waliivamia Afghanistan mwaka 2001 ikiwa ni katika sehemu ya kile kilichotajwa kuwa vita dhidi ya ugaidi. Licha ya kuiondoa madarakani serikali ya kundi la Taliban, machafuko na umwagaji damu unaendelea kushuhudiwa nchini Afghanistan tangu wakati huo hadi sasa pamoja na kuweko maelfu ya askari wa majeshi ya kigeni yanayoongozwa na Marekani

RAIS WA UJERUMANI ASEMA SNOWDERN ANASTAHILI HESHIMA

Rais wa Ujerumani Joachim Gauck ametoa ujumbe wa kumuunga mkono Edward Snowden, mfanyakazi wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani CIA aliyefichua siri za ujasusi unaofanywa na shirika hilo kuwa ni mtu anayestahili heshima kwa kutetea uhuru wa faragha wa mtu binafsi. Gauck ametoa kauli hiyo katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti moja la Ujerumani. “Mtu yeyote anayetoa taarifa kwa umma na kuchukua hatua kutokana na dhamiri ya nafsi yake anastahili heshima”, amesema Rais huyo wa Ujerumani. Ameongeza kuwa tangu mwezi uliopita wa Juni wakati Snowden alipofichua taarifa za shughuli za ujasusi unaofanywa na Marekani, binafsi amekuwa na mashaka makubwa na wasiwasi wa kuchelea kama kuna usalama kwa yeye kutuma barua pepe na kuzungumza kwa uwazi kabisa kwa kutumia njia ya simu. Rais wa Ujerumani ameongeza kama ninavyomnukuu: “hofu ya kuchelea kunaswa na kuhifadhiwa na mashirika ya kigeni ya ujasusi mazungumzo yetu ya simu au barua pepe yanabana hisia zetu za kujihisi kuwa tuko huru na wenye faragha”. Rais wa Ujerumani ameitaka serikali ya Kansela wa nchi hiyo Angela Merkel ifikie makubaliano na waitifaki wake yatakayoheshimiwa ya kudhamini uhuru wa faragha wa watu. Edward Snowden alifichua kuwa mashirika ya ujasusi ya Marekani hufanya udukuzi kote duniani kwa kutumia mbinu ya kiteknolojia ya siri kuchunguza mawasiliano ya simu ya watu, barua pepe na mawasiliano mengine

Friday, July 26, 2013

MAHAKAMA ISRAEL YARUHUSU KUTUMIWA SILAHA ZA KEMIKALI

Waziri wa Afya wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina inayoongozwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amelaani vikali hatua ya Mahakama Kuu ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuruhusu utumiwaji gesi ya kemikali yenye mada za fosforasi nyeupe. Mufid al Mukhlalati amesema kuwa, hatua ya mahakama hiyo kuruhusu utumiwaji wa gesi hizo za kemikali zenye mada za fosforasi nyeupe, kunalipa nguvu jeshi la utawala huu kutengeneza silaha hatari za kemikali zitakazotumiwa dhidi ya wananchi wa Palestina. Tarehe 9 Julai mwaka huu, Mahakama Kuu ya Israel ilitangaza kuwa, utumiwaji wa gesi hiyo ya kemikali ni ruhusa kabisa. Waziri wa Afya wa Palestina amesema kuwa, hivi sasa mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yanafanya juhudi za kuzuia jinai zinazofanyika ulimwenguni kote, lakini vyombo vya sheria vya utawala wa Israel vinapuuzia sheria za kimataifa kwa kuruhusu utumiwaji wa gesi za kemikali zenye mada za fosforasi nyeupe.

UN YALAANI SERA ZA ISRAEL KUCHUKUA ARDHI ZA PALESTINA

Navi Pillay Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kuufanyia mabadiliko mswada wa sheria ambao ikiwa utatekelezwa utasababisha kuporwa kwa ardhi katika eneo la Negev na hivyo kupelekea watu takribani 40,000 kutoka jamii ya Bedouin kutimuliwa kutoka kwenye ardhi ya mababu zao.
Pillay anasema kuwa 'watu wa jamii ya Bedouin wana haki sawa ya kumiliki mali, nyumba na kupata huduma za umma kama jamii nyingine yeyote ile ya Israel'. Pillay alielezea masikikitiko yake kuwa bado utawala wa Israel unaendelea kuwalazimu watu wenye asili ya Kiarabu kuhama makwao hata baada ya kulizungumzia suala hilo alipofanya ziara Israel miaka miwili iliyopita. Pillay ameongeza kuwa ikiwa mswada huo utakuwa sheria utachochea kubomolewa kwa makao ya jamii hiyo na kuwalazimu watu hao kuhama makwao hatua ambayo itawanyima haki yao ya kumiliki ardhi.

HANIA ALAANI PROPAGANDA ZA WAARABU

Waziri Mkuu wa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina amelaani vikali propaganda za baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu dhidi ya taifa la Palestina. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Waziri Mkuu, Ismail Hania, sambamba na kulaani propaganda hizo zinazofanywa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu imetangaza kuwa, madai ya vyombo hivyo vya habari kwamba, Wapalestina na Muqawama wa Palestina ulikuwa na nafasi katika matukio ya Misri ni uongo wa wazi ambao ni kwa maslahi ya utawala haramu wa Israel. Wakati huo huo, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani hukumu ya mahakama moja nchini Misri ya kuendelea kumshikilia Muhammad Mursi, Rais aliyeondolewa madarakani nchini humo kwa tuhuma za kushirikiana na harakati ya Hamas ya Palestina. Sami Abu Zuhri, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, maana ya uamuzi huo ni kuwa harakati hiyo ni adui wa taifa la Misri.

KATIBU WA UN ATAKA MORSI AACHIWE HURU

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ametoa wito kwa Serikali ya Misri kumuachia Kiongozi aliyeondolewa madarakani kwa nguvu za Jeshi Mohamed Morsi kipindi hiki nchi hiyo ikijiandaa kufanya maandamano ya kitaifa yaliyoitishwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Abdel Fattah Al Sisi. Ban amesema wakati wa kuachiwa kwa Morsi umefika na iwapo anapaswa kujibu mashtaka yoyote ni bora kitu hicho kifanyike kwa uwazi ili kumaliza hali ya wasiwasi ambao imeendelea kushuhudiwa nchini Misri kutokana na wafuasi wake kupiga kambi mitaani wakifanya maandamano. Katibu Mkuu wa UN ameweka wazi iwapo Morsi ataendelea kushikiliwa basi itakuwa vigumu kwa nchi hiyo kushuhudia utulivu wa dhati ambao ulikuwepo hapo awali baada ya kuchaguliwa kidemokrasia Kiongozi huyo na kukaa madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja. Morsi na Viongozi wengine kadhaa wa Chama Cha Muslim Brotherhood wangali wakishikiliwa na Serikali inayoongozwa na Kiongozi wa Mpito Adly Mahmud Mansour ambaye amepewa jukumu la kuitisha uchaguzi mapema mwakani ili demokrasia ichukue mkondo wake.
Kitendo hicho cha kuendelea kushikiliwa kwa Morsi na Viongozi wengine wa Chama Cha Muslim Brotherhood ndicho kinaonekana chanzo cha uwepo wa maandamano yasiyokishwa kutoka kwa wafuasi wa Chama hicho waliojiapiza kuendelea kupambana hadi pale Kiongozi wao atakaporudishwa madarakani. Wito wa Ban unakuja kipindi hiki wafuasi wanaopinga Chama Cha Muslim Brotherhood wakijiandaa kufanya maandamano makubwa kuunga mkono serikali mpya na kutoa kibali kwa jeshi kupambana na machafuko yanayoendelea sanjari na vitendo vya kigaidi vinavyoshuhudiwa. Maandamano hayo ya Kitaifa yaliitishwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Al Sisi ambaye alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuonesha wanaunga mkono juhudi za jeshi katika kuzima vitendo vyote vy akigaidi vinavyoendelea. Viongozi kadhaa wa zamani nchini Misri wamekosoa maandamano hayo akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Hisham Qandil ambaye ameonya hatua hiyo akisema huenda ikachochea zaidi machafuko katika Taifa hilo. Naye Kiongozi wa Chama Cha Muslim Brotherhood Mohamed Badie amesema maandamano hayo hayatosaidia kurejesha utulivu na badala yake ametoa wito kwa wananchi kusimama kupigania uhuru na kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliyomwaga damu.

TAKWIMU ZA UMOJA WA MATAIFA ZAONYESHA WATU ZAIDI YA 100,000 WAMEFARIKI SYRIA

Umoja wa Mataifa UN umetoa takwimu zinazoonesha watu zaidi ya 100,000 wamepoteza maisha nchini Syria tangu kuzuka kwa mapigano kati ya Wapinzani na Jeshi linalomtii Rais Bashar Al Assad yaliyodumu kwa zaidi ya miezi ishirini na nane sasa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amesema watu zaidi ya laki moja wamepoteza huku wengine mamilioni wakilazimika kuyakimbia makazi yao wakijiepusha na madhara ya vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe. Ban amekiri ongezeko hilo la vifo limeendelea kuleta hofu juu ya hali ya usalama wa baadaye wa Syria kutokana na mapigano baina ya Wapiganaji wa Wapinzani na Jeshi la Serikali ya Damascus kuendelea kushika kasi.
Katibu Mkuu wa UN amesisitiza mapigano hayo yamechangia mzigo wa wakimbizi kwa mataifa jirani ambayo yamelazimika kuendelea kupokea watu hao wanaokimbia machafuko kwa sasa. Ban ametoa wito kwa Marekani na Urusi kuhakikisha wanafanya kila linalowezekana ili mazungumzo ya Geneva yafanyike na kuzileta pamoja pande zinazohasimiana nchini humo kwa zaidi ya miaka miwili. Katibu Mkuu Ban amesisitiza mazungumzo ndiyo njia pekee ambayo inaweza ikasaidia kupatika kwa suluhu nchini Syria na hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe vikamalizwa. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema wanafanya kila linalowezekana wakishirikiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergie Lavrov kuhakikisha mazungumzo ya Geneva yanafanyika. Kerry ameweka bayana lengo lao ni kuhakikisha Serikali ya Damascus na Wapinzani wanafika kwenye meza ya mazungumzo huko Geneva ili kusaka suluhu ya kudumu ya machafuko hayo. Katika hatua nyingine Kiongozi wa Baraza la Upinzani nchini Syria SNC Ahmad Jarba ametoa wito kwa Marekani kuwapatia msaada wa kijeshi ili waweze kuendelea na mapigano dhidi ya Jeshi la Serikali.
jarba ametoa kauli hiyo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Kerry na kumueleza wanahitaji msaada wa haraka wa silaha kitu ambacho kitawasaidia kusonga mbele kwenye mapigano hayo. Haya yanakuja kipindi hiki mapigano makali yakiendelea kushuhudiwa katika Mji wa Homs ambao unashikiliwa na Wapinzani huku Jeshi la Rais Assad likihaha kuhakikisha linaukomboa.

WAASI DARFUR WASHAMBULIA WANAJESHI

Waasi kutoka jimbo la Darfur nchini Sudan, wameshambulia kambi ya jeshi Kaskazini mwa Kordofan, na kuwaua wanajeshi 5 katika makabiliano makali . Hii ni kwa mujibu wa jeshi la nchi hiyo. Eneo la Kordofan Kaskazini halijakuwa likishuhudia mashambulizi kutokana na vurugu katika jimbo la Darfur karibu na mpaka na Sudan Kusini. Sudan Kusini imekana madai kuwa inaunga mkono waasi wa Darfur. Maelezo zaidi kuhusu mapigano hayo bado hayako wazi, ingawa makabiliano haya yanakuja kabla ya makataa ya kusitisha usafirishaji wa mafuta kutoka Sudan Kusini kutokana na madai ya kuunga waasi mkono.
Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011, chini ya mkataba wa mwaka 2005 wa kukomesha mapigano yaliyodumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika. Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, uhusiano kati ya majirani hao wawili umezorota kuhusu mapato ya mafuta na tuhuma kuwa pande zote zinaunga mkono waasi kupiga mwingine. Waasi waliopigana vita vya Sudan Kusini wakati wa mapigano, walijipata upande wa mpaka wa Sudan baada ya nchi hiyo kujitenga na kisha wakachukua silaha kupigana wakidai kuwa maslahi yao bado hayatimizwi. Pamoja na makundi matatu ya waasi katika jimbo la Darfur, waliungana na kubuni kikundi cha waasi cha Sudan Revolutionary Front na wamekuwa wakiendesha harakati zao katika maeneo ya Kordofan ya Kusini na Blue Nile, ambayo yanapakana na Sudan Kusini.

MAREKANI YAAMUA KUCHELEWESHA KUPELEKA NDEGE MISRI

Marekani imesema kuwa itachelewesha mpango wake wa kuikabidhi Misri ndege za kivita aina ya F-16 huku mgogoro wa kisiasa ukiendelea kutokota nchini Misri kufuatia kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Mohammed Morsi. Msemaji wa idara ya ulinzi nchini Marekani, George Little alisema kuwa uamuzi huo ulifikiwa kutokana na hali inayokabili Misri kwa sasa. Marekani inadadisi ikiwa kuondolewa mamlakani kwa Morsi ilikuwa mapinduzi ya kijeshi, hali inayoweza kusababisha Marekani kusitisha msaada wake kwa Misri.
Hapo jana mkuu wa jeshi la Misri Generali Sisi , aliitisha maandamano ya umma akiwataka wananchi kuliruhusu jeshi kukabiliana na kile alichokiita tisho la ugaidi. Lakini Abdel Fattah al-Sisi aliongeza kuwa hakuwa anaitisha maandamano kwa lengo la vurugu huku akiwasihi wananchi kuwa na maridhiano. Katika jibu lake kwa wito wa jeshi, chama cha Muslim Brotherhood, ambacho kinamuunga mkono Morsi, kilisema kuwa Generali Sisi alikuwa anaitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ndege hizo nne aina ya F-16 ni sehemu ya ndege nyingine 20 ambazo zimeitishwa, kati ya hizo nane tayari zikiwa zimepelekwa Misri. Hata hivyo Marekani iliahidi tarehe 11 mwezi Julai kuwa bado ina mpango wa kuikabidhi Misri ndege hizo.

JESHI HISPANIA LAMHOJI DEREVA WA TRENI ILIYOPATA AJALI

Jeshi la Polisi nchini Uhispani linatarajiwa kuanza kumhoji mmoja wa madereva wa garimoshi lililopata ajali nchini humo na kuchangia vifo vya abiria wanaokadiriwa kufikia themanini na kuwaacha wengine zaidi ya mia moja thelathini wakijeruhiwa. Jeshi limesema kuwa mahojiano hayo ni sehemu ya uchunguzi ulianza kufanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo mbaya zaidi ya garimoshi kutokea katika kipindi cha miaka 40 nchini humo. Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema miongoni mwa vitu ambavyo watahitaji kujiridhisha navyo ni pamoja na kufanya uhakiki ili kujua kama kweli kama garimoshi hilo lilikuwa kwenye mwendokasi mara mbili ya uliopaswa. Vyombo vya Habari nchini Uhispania viliandika moja ya chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo ni mwendo kasi mara mbili iliyokuwa inaenda na kuchangia kutoka kwenye njia yake ya reli kabla ya kupata ajali hiyo.
Shirika la Reli la Taifa nchini Uhispania linalotambulika kwa jina la Renfe limeweka wazi ni mapema sana kusema mwendo kasi ni chanzo cha ajali hiyo mbaya katika taifa hilo na hivyo uchunguzi wa kina unapaswa kufanyika. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Usafirishaji nchini Uhispania Rafael Catala amesisitiza dalili za awali zinathibitsha mwendeo kasi unaweza ukawa ulichangia ajali hiyo kwa mujibu wa picha za CCTV zilizorekodi tukio hilo. Mfalme wa Uhispania Juan Cralos amewatembelea majeruhi wa ajali hiyo ya garimoshi na kusema wananchi wanapaswa kuungana kipindi hiki ambacho uchunguzi unafanywa kubaini sababu ya janga hilo la kitaifa.
Mfalme Carlos amekiri kila mwananchi wa Uhispania ameumizwa na ajali hiyo iliyotokea katika Jiji la Santiago de Compostela na hivyo huu si wakati wa kuanza kunyosheana vidole vya lawama. Waziri Mkuu Mariano Rajoy ameteua tume mbili ambazo zinajukumu la kufanya uchunguzi kubaini sababu za kutokea kwa ajali hiyo huku pia akitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

MGOMO WAFANYIKA TUNISIA KUPINGA KIFO CHA MBUNGE WA UPINZANI

Mgomo wa Kitaifa umeitishwa nchini Tunisia ukiwa na lengo la kuonesha kukasirishwa na hatua kuuawa kwa Mbunge wa Upinzani nchini humo Mohamed Brahmi ambaye anatajwa alikuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Chama Cha Ennahda. Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi nchini Tunisia UGTT limeitisha mgomo wa kitaifa utakaoambatana na m,aandamano kuonesha kuchukizwa kwao na mauaji ya Mbunge Brahim. Brahmi alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake na watu waliokuwa wamejihami na silaha na hadi sasa hawajulikani kina nani na hakuna Kundi lolote ambalo limejitangaza kutekeleza mauaji hayo. Maandamano makubwa yalishuhudiwa usiku wa alhamisi kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Tunis kushinikiza Jumuiya ya Kimataifa kulaani kile ambacho kimefanywa huku wengi wakinyoosha kidole cha lawama kwa Serikali.
Shirika la Ndege nchini humo la Tunisair limetangaza kufuta safari zake zote za ndege kitu ambacho kinatajwa kitaathiri shughuli nyingi ikiwa ni sehemu ya kuonesha kupinga kwao mauaji hao ya Brahmi. Chama Tawala cha Ennahda kimejitenga na mauaji hayo ya Mbunge Brahmi na kusema madai ambayo yanatolewa na familia kuwalenga wao kupanga na kutekeleza tukio hilo hayana ukweli wowote. Jeshi la Polisi limekuwa kwenye kibarua kizito cha kupambana na waandamanaji waliojitokeza kwenye mitaa ya Tunis na Sidi Bouzid eneo ambalo linatajwa kuwa chanzo cha mapinduzi yaliyomuangusha Rais Zine El Abidine Ben Ali. Brahmi mtu ambaye alikuwa na mrengo wa kushoto anakumbukwa vyema kwa kuanzisha maandamano makubwa ya kitaifa ya saa mbili yaliyosababisha kuangushwa kwa Utawala wa Ben Ali.
Dada wa Marehemu Chhiba Brahmi amekituhumu waziwazi Chama Tawala cha Ennahda kuhusika na mauaji ya ndugu yao na wametaka uchunguzi huru ufanyike kubaini waliohusika kwenye tukio hilo. Mkuu wa Chama Cha Ennahda Rached Ghannouchi amekanusha kwa nguvu zake zote madai ya kwamba wao ndiyo wamehusika kwenye mauaji ya Brahim na kusisitiza mauaji hayo ni janga kwa Tunisia. Mohamed Brahim anakuwa mwanasiasa wa pili kuuawa nchini Tunisia baada ya mwezi februari kutekelezwa mauaji ya mwanasiasa mwingine wa upinzani Chokri Belaid aliyeuawa nje ya nyumba yake.
Marekani imelaani mauaji hayo huku Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya EU Catherine Ashton akitoa tamko hilo hilo wakati Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kutetea Haki za Binadamu Navi Pillay akitaka uchunguzi wa haraka ufanyike.

Thursday, July 25, 2013

AJALI YA TRENI YATOKEA HISPANIA NA KUUWA WATU KADHAA


A train has derailed in north-western Spain, killing at least 77 people and injuring more than 100, officials in the Galicia region have said. All eight carriages of the train, which was travelling from Madrid to Ferrol, came off the tracks near the city of Santiago de Compostela.
Rescue workers continued to search for survivors in the train wreckage through the night.
Analysts say it is the worst rail accident in Spain in four decades. Rescue workers have so far recovered 73 bodies from the accident site, while four more people died in hospital, a spokeswoman for Galicia's supreme court said on Thursday. Judges are responsible for registering deaths in Spain.

WAISLAM UK WATAKA KUKABILIWA KWA MASHAMBULIZI DHIDI YAO

Jumuiya kubwa zaidi ya Kiislamu nchini Uingereza, imetaka kuchukuliwa hatua na mikakati ya pamoja kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Katika barua kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza, Faruq Murad Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini humo, ameashiria ongezeko la mashambulizi dhidi ya Waislamu na kuitaka serikali na vikosi vya polisi nchini humo kuchukua hatua ya pamoja katika kuzuia hujuma hizo dhidi ya Waislamu. Baada ya kuuawa askari mmoja wa nchi hiyo na watu wawili mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, makundi yenye kufurutu mipaka ya mrengo wa kulia, yalitumia vibaya mauaji hayo kushadidisha vitendo vya kikatili dhidi ya Waislamu. Tokea wakati huo, misikiti na makaburi ya Waislamu hayajasalimika na mashambulizi ya makundi hayo wenye misimamo ya kufurutu mipaka. Vitendo vya ubaguzi dhidi ya Uislamu na kukanyagwa haki za Waislamu, vimeshtadi sana nchini humo. Aidha ongezeko la propaganda chafu za vyombo vya habari vya Uingereza, linatajwa kuwa sababu ya kushtadi ubaguzi dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Vitendo vya kufurutu mipaka vinavyofanywa na magenge ya magaidi, vimekuwa chanzo na sababu ya makundi ya mrengo wa kulia yenye kufurutu mipaka na serikali ya London, kushadidisha mashinikizo na sheria kali dhidi ya Waislamu. Hata hivyo propaganda hizo na hatua za kibaguzi dhidi ya Uislamu, zimekabiliwa na radiamali kali kutoka kwa makundi yanayopinga ubaguzi wa rangi, vita na ya kutetea haki za binaadamu nchini Uingereza. Pamoja na taasisi na jumuiya za Kiislamu kulaani vikali mauaji ya mwezi Mei dhidi ya askari wa nchi hiyo, lakini bado propaganda dhidi ya Uislamu zingali zinaendelea katika baadhi ya vyombo vya habari vya nchi hiyo ya Ulaya. Aidha ubaguzi dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa ujumla umeongezeka katika fikra za waliowengi, licha ya viongozi wa Uingereza akiwemo David Cameron Waziri Mkuu wa nchi hiyo, kutoa azimio lililo wazi la kuwataka wananchi kudumisha umoja na kusisitiza kutohusika Waislamu katika mauaji ya askari huyo. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, serikali ya London na vyombo vya habari vya nchi hiyo, vimekuwa vikiendesha kampeni za kibaguzi kwa muda mrefu dhidi ya Uislamu hususan baada ya tukio la Septemba 11 nchini Marekani. Ni kwa ajili hiyo, ndio maana muungano wa Kiislamu nchini humo, ukaitaka serikali hiyo, kuzuia mashambulzi dhidi ya Waislamu na vituo vyao vya ibada, mashambulizi ambayo kwa hakika yanafanyika kwa baraka za serikali na polisi ya nchi hiyo.

WALIOTOROKA JELA IRAQ KWENDA SYRIA

Kundi la kigaidi la al-Qaida la nchini Iraq limetangaza kuhusika na hujuma dhidi ya magereza ya Abu Ghureib na Taji ambapo zaidi ya wafungwa 500 walitoroka. Taarifa ya al-Qaeda imesema wafungwa hao wako tayari kupigana na serikali ya Rais Bashar Asad wa Syria na kwamba mipango inafanywa ili waelekee nchini humo. Katika hujuma hiyo kwenye magereza hayo mawili makubwa nchini Iraq, zaidi ya watu 50 waliuawa wakiwemo maafisa wa gereza huku wengine wengi wakijeruhiwa. Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki amesema serikali yake itaendelea kukabiliana na magaidi na kwamba juhudi za kuwasaka wafungwa waliotoroka zinaendelea. Imebainika kwamba baadhi ya walinzi kwenye gereza la Abu Ghureib walishirikiana na magaidi kwenye hujuma hiyo iliyotokea Jumapili iliyopita.

ZAMBIA YASEMA TOKA ULAYA INA KEMIKALI ZA SARATANI

Zambia imesitisha uagiziaji wa nyama ya ng'ombe kutoka bara Ulaya baada ya kubainika ina kemikali inayosababisha ugonjwa hatari wa saratani.BShirika kubwa zaidi la nyama ya ng'ombe Zambia, Zambeef, leo limetoa taarifa likisema, mada ya kemikali ijulikanayo kama aromatic aldehydes imepatikana katika nyama kutoka Ulaya hasa Uingereza.
Zambeef ilikusanya bidhaa zote za nyama ya ng'ombe katika maduka yake baada ya kubainika kuwepo kemikali hiyo ambayo pia hutumiwa kuhifadhi maiti. Mkurugenzi wa Zambeef Jacob Mwanza amesema kuanzia sasa shirika hilo litakuwa likinunua nyama ya ngo'ombe kutoka Zambia pekee. Katika miaka ya hivi karibuni nchi za Ulaya zimelaumiwa kuwa zinazitumia nchi za Afrika kama jalala la bidhaa ambazo zimepigwa marufuku barani humo.

FAMILIA YA MORSI YASHUTUMU JESHI KUMTEKA MORSI

Mwanawe wa kike aliyekuwa rais wa Misri na ambaye alipinduliwa na jeshi, Mohamed Morsi ametuhumu jeshi kwa kumteka babake. Katika taarifa ya kwanza ya familia ya Morsi tangu kung'olewa kwake na jeshi mapema mwezi huu, Shaimaa Mohamed Morsi aliwaambia waandishi wa habari kuwa familia yake itamuhoji mkuu wa jeshi Generali Abdel Fattah al-Sisi, ikiwa chochote kitamtendekea babake.
Alisema kuwa familia yake itaiomba mahakama ya kimatifa ya uhalifu wa kivita kufanya uchunguzi katika kile alichokiita mapinduzi ya kijeshi yaliyosababisha mauaji na umwagikaji wa damu.Mawakili wa Morsi  walisema kuwa ni ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu kwa kuwa anakamatwa bila makosa.

WAASI SYRIA WAKIRI KUPATA PIGO KUBWA

Kamanda wa kundi la waasi nchini Syria amekiri kwamba jeshi la serikali ya Syria limepiga hatua kubwa katika kuyakomboa maeneo mbalimbali yaliyokuwa yakidhibitiwa na waasi hao nchini humo. Salim Idriss kamanda wa kikundi kinachojiita "Jeshi la Ukombozi wa Syria' amesema leo kuwa, makundi ya waasi yamevunjwa moyo na msimamo wa nchi za Ulaya na Marekani, wa kukataa kutuma silaha kwa makundi ya waasi na magaidi nchini Syria na kusisitiza kuwa, suala hilo limepelekea jeshi la Syria kusonga mbele na kuyakomboa maeneo mengi nchini humo. Kamanda wa kundi la kigaidi la Jeshi la Ukombozi wa Syria amezikosoa siasa za kindumakuwili za nchi za Magharibi na Marekani kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za kuwapelekea silaha waasi wa Syria. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Uingereza  ilikuwa mstari wa mbele kuzishawishi nchi nyingine za Ulaya kuwapelekea silaha waasi na magaidi wa Syria, lakini mkakati huo ulifeli baada ya makamanda wa jeshi la Uingereza kumuonya David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza.

JENERALI AL-SISI ATAKA WANANCHI KUFANYA MAANDAMANO MAKUBWA IJUMAA

Mkuu wa Majeshi nchini Misri Jenerali Abdel Fattah Al Sisi ametoa wito wa kufanyika ya kitaifa ambayo yatampa mamlaka yeye ya kupambana na vitendo vya ugaidi pamoja na machafukoyanyoendelea kushuhudiwa kipindi hiki wafuasi wa Mohamed Morsi wakipinga kitisho hicho. Jenerali Al Sisi ametoa tamko hilo kupitia hotuba yake iliyorushwa kupitia Televisheni ya Taifa akiwahamasisha wananchi wa Misri kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano ya kitaifa ambayo ametaka yafanyike siku ya Ijumaa ikiwa ni ishara ya kumpa fursa ya kukabiliana na vitendo vinavyokwenda kinyume cha sheria. Kiongozi huyo wa Kijeshi ambaye aliongoza mchakato wa kumuondoa madarakani Morsi tarehe 3 ya mwezi Julai amesema anahitaji uungwaji mkono kutoka kwa wananchi wa Misri ili aweze kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na vitendo vya kigaidi vilivyoanza kuchomoza.
Wito wa Jenerali Al Sisi unakuja kipindi hiki ambacho wafuasi wa Morsi wameendelea kufanya mashambulizi wakishinikiza kuachiwa kwa Kiongozi huyo wa Chama Cha Muslim Brotherhood ambaye yupo chini ya uangalizi wa Jeshi tangu aondolewe madarakani mapema mwezi huu. Jenerali Al Sisi ameweka wazi nia yake ni kupambana na machafuko pamoja na vitendo vyote vya kigaidi vinavyofanyika nchini Misri ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa mashambulizi yanayotekelezwa kwa kutumia mabomu. Kiongozi huyo wa Kijeshi nchini Misri amesema kumekuwa na machafuko yanayoendelea kila uchao yanayoratibiwa na Makundi ya watu wenye silaha kitu ambacho kinachangia kuzorotesha hali ya usalama wa Taifa hilo.
Jenerali Al Sisi amekanusha vikali madai ya kwamba amemsaliti Mohamed Morsi aliyemteua kushika wadhifa huo na badala yake amesema Kiongozi yoyote anapaswa kuongozwa kwa misingi inayoridhiwa na wananchi na si kinyume na hapo. Takwimu zinaonesha watu zaidi ya 200 wameshapoteza maisha nchini Misri tangu Morsi aondolewe madarakani na Jeshi ambapo wafuasi wa Chama chake cha Muslim Brotherhood wakajitokeza mitaani wakijiapiza kushinikiza arudishwe madarakani. Viongozi wa Chama Cha Muslim Brotherhood amesema hawatatishwa na kalu ya Jenerali Al Sisi na badala yake wataendeleza maandamano yao hadi pale ambapo Kiongozi wao ataachiwa na kukabidhiwa madaraka aliyoporwa. Chama Cha Muslim Brotherhood kimetoa wito kwa wafuasi wake kutorudi nyuma na badala yake kuongeza shinikizo na kushikilia msimamo wao hadi pale sauti zao zitasikika na Mohamed Morsi kukabidhiwa wadhifa wake alioupata kwa njia za kidemokrasia.

URUSI YAMPA KIOBALI CHA KUSAFIRI SNOWDERN

Serikali ya Urusi imetoa nyaraka kwa Mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Kijasusi nchini Marekani CIA Edward Snowden zinazomruhusu kuondoka katika eneo la Uwanja Ndege ambalo amekuwa akiishi tangu awasili akitoke China. Shirika la Habari la Umma la Urusi RIA limethibitisha kupatiwa kwa nyaraka hizo kwa Snowden ambaye amekuwa akihaha kuomba hifadhi kipindi hiki akisakwa kwa udi na uvumba na Serikali ya Marekani baada ya kuvujisha siri za Shirika la CIA. Nyaraka hizo zimetoa nafasi kwa Snpwden kuweza kuingia nchini Urusi na kuomba hifadhi ay hata kuondoka na kueleka katika nchi yoyote ambayo itakuwa tayari kumhifadhi bila ya walinzi wa mpaka kumzuia. Taarifa zinasema baada ya Snowden kupatiwa nyaraka hizo muhimu anatazamia wakati wowote ataondoka katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Moscow alipokuwa anahifadhiwa sehemu ya abiria wanaopita nchi hiyo kueleka mataifa mengine.
Snowden amepata nyaraka hizo muhimu kutoka kwa usaidizi wa Mwanasheria wake Anatoly Kucherena ambaye amekwenda katika Uwanja wa Ndega wa Sheremetyevo kukutana na mteja wake. Nyaraka hizo amekabidhiwa Kucherena ambaye ndiye atamkabidhi Snowden anayetajwa tayari ameshabadilishiwa hadi mavazi yake tayari kwa kuingia nchini Urusi na kuendelea na mchakato wa kuomba hifadhi ya kudumu. Mwanasheria wa Snowden, Kucherena amesema iwapo mteja wake atakuwa tayari kupatiwa uraia wa Urusi atafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha anapata nafasi hiyo ambayo huenda ikatolewa kwake bila pingamizi.
Mapema mwezi huu Snowden alijitokeza na kuomba hifadhi nchini Urusi ambapo aliambiwa mchakato wa yeye kupewa hadhi huyo huenda ungechukua hata kipindi cha miezi mitatu kabla ya kukubaliwa. Mfanyakazi huyo wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Nchini Marekani CIA Edward Snowden amekuwa akippata hifadhi ya muda nchini Urusi kitu ambacho kimechangia kuleta mgogoro wa uhusiano baina ya Serikali za Washington na Moscow.

Wednesday, July 24, 2013

ARBOUR ASEMA ICC IMEPOTEZA MWELEKEO WAKE

Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la kimataifa la migogoro amesema kuwa, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilifanya makosa kutoa tuhuma  za kutenda  jinai za kivita na kibinadamu dhidi ya Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan. Louise Arbour ambaye alishawahi kuwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa na mjumbe wa kamati ya kimataifa ya uchunguzi huko Darfur magharibi mwa Sudan amesema kuwa, tuhuma zilizotolewa dhidi ya Rais al Bashir zimeidhoofisha nafasi ya mahakama ya ICC. Mahakama hiyo yenye makao yake The Hague nchini Uholanzi inamtuhumu Rais al Bashir kwa kutenda jinai za kivita na kibinadamu na imezitaka nchi za Kiafrika kumtia mbaroni  kiongozi huyo pindi atakapozitembelea nchi hizo. Hata hivyo, kikao cha wakuu wa Umoja wa Afrika kilichofanyika mwaka 2009 huko Sirte nchini Libya, kilichukua uamuzi wa pamoja wa kutoshirikiana na mahakama kuhusiana na mpango wa kumtia mbaroni Rais wa Sudan.

KIONGOZI MWANDAMIZI WA HAMAS APINGA MAZUNGUMZO NA ISRAEL

Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameukosoa vikali uamuzi wa Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina wa kukubali kufanya mazungumzo ya mapatano na utawala haramu wa Israel na kusema hatua hiyo ni  sawa na kujiua kisiasa. Usama Hamdan amesisitiza kwamba, kufanya mazungumzo ya mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel hakuna natija yoyote ghairi ya kupoteza haki za Wapalestina na kimsingi ni kutoa pigo kwa kadhia nzima ya Palestina. Kiongozi huyo mwandamizi wa Hamas amemkosoa vikali Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kubainisha kwamba, daima Mahmoud Abbas amekuwa akisema kuwa, anafungamana na misingi thabiti ya Wapalestina, lakini katika vitendo hafungamani na misingi hiyo. Usama Hamdan ameongeza kuwa, kushiriki katika mazungumzo ya mapatano ya Washington sio tu kwamba, ni ujinga wa kisiasa bali ni kujiua kisiasa na kupoteza haki za wazi za Wapalestina. Amesema, kufanyika mazungumzo kama hayo hakuna wakati ambao yatazuia kuendelea jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina sambamba na kuvunjiwa heshima matukufu yao.

GAZETI LA UINGEREZA LACHAPISHA WAISLAM KUWA WATU WAKARIMU ZAIDI

Gazeti la Times linalochapishwa nchini Uingereza limeitaja dini tukufu ya Kiislamu kuwa ni dini yenye kutilia umuhimu mkubwa suala la  kuwalingania watu katika kutoa walichonacho na kwamba wafuasi wa dini hiyo tukufu ndio watu wakarimu zaidi kati ya wananchi wa Uingereza.  Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la Times kwa kushirikiana na kituo cha mawasiliano cha 'Just Giving' kwa watu elfu nne nchini Uingereza unaonyesha kuwa, Waislamu nchini humo ni wakarimu zaidi kuliko wafuasi wa dini nyingine. Imeelezwa kuwa, Waislamu wamekuwa wakitoa misaada yao ya kibinadamu kupitia taasisi  kama vile 'Islamic Relief'  na 'Muslim Aid' kwa watu wenye kuhitaji misaada na pia hupeleka misaada kwa taasisi zisizokuwa za Kiislamu kama vile taasisi za kusaidia wagonjwa wa  maradhi ya saratani nchini humo.

NJAMA ZA KUMPINDUA RAIS KABILA

Raia kumi na tisa wa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo wanaoshukiwa kuwa waasi wamefunguliwa mashtaka nchini Afrika Kusini kwa njama ya kutaka kuipindua serikali ya Rais Joseph Kabila
Wendesha mashtaka walisema kuwa washukiwa hao ni wanachama wa kundi la waasi la (Union of Nationalists for Renewal, UNR, nchini DRC. Polisi wa kupambana na ugaidi waliwakamata washukiwa hao katika mkoa wa kaskazini, Limpopo. Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imekumbwa na uasi wakati wote wa utawala wa Kabila.
Aliingia mamlakani mwaka 2001,baada ya mauaji ya babake, Laurent Kabila.Mmoja wa washukiwa wa njama ya mapinduzi ametambuliwa kama raia wa Marekani James Kazongo, kulingana na ripoti za shirika la habari la AP.''Washukiwa hao waliingia Afrika Kusini kupanga mafunzo maalum ya kijeshi kwa lengo la kumpindua rais Kabila,'' alisema kiongozi wa mashtaka Shaun Abrahams. ''Walikuwa wameahidi kuwokodisha mamluki ambao wangewalipa kwa kuwapa migodi ya dhababau nchini DRC,'' alisema bwana Abrahams.Polisi nchini walipokea taarifa kuhusu kuwepo nchini humo kwa washukiwa hao, mwezi Septemba mwaka jana. Kuna makundi mengi ya waasi wanaoendeshea harakati zao Mashariki mwa DRC.
Eeneo hilo limeathirika kutokana na uasi wa kundi la M23 ambalo limelazimisha takriban watu laki nane kutoroka makwao.

GHASIA ZAIBUKA BRAZIL KATIKA MAPOKEZI YA PAPA

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amepokelewa kwa shangwe nchini Brazil ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi ya nje tangu apate nafasi hiyo na ameianza katika nchi ambayo inatajwa kuwa na waumini wengi zaidi wa kanisa hilo Duniani. Papa Francis amepata mapokezi hayo ya kipekee licha ya kwamba katika baadhi ya maeneo kumekuwa na maandamano yaliyoambatana na ghasia kupinga ujio wake nchini Brazil kitu kilichowapa wakati mgumu askari. Jeshi nchini Brazil lilikuwa na kibarua kigumu kukabiliana na waandamanaji hao ambao wanakosoa kufanyika kwa ziara hiyo ya Papa Francis nchini humo wakidai nchi hiyo imeshindwa kusikiliza matakwa ya wananchi wake.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba bendera za taifa la Brazil pamoja na kuimba nyimbo mbalimbali wamejitokeza kwenye mitaa ya Jiji la Rio De Janeiro kitu kilichochangia Jeshi kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya. Waandamanaji hao walikuwa wanashinikiza kusikilizwa ili watume ujumbe wao kwa Papa Francis alipokuwa anakutana na Rais Dilma Rousseff ambaye akikabiliwa na maandamano ya kukosoa sera zake katika kuboresha maisha ya wananchi. Wananchi hao waliojitokeza mitaani wameendelea kushinikiza Rais Rousseff kuondoka madarakani kutokana na kushindwa kuboresha maisha ya wananchi wake tangi aingie madarakani kitu kilichochangia hali ngumu ya maisha. Licha ya uwepo wa maandamano na ukosoaji dhidi ya ziara hiyo ya juma moja ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani nchini Brazil Papa Francis kuna wale ambao walijitokeza na kufurahia ujio wake.
Wengi waliojitokeza kumpokea Papa Francis wamesema hii ni ziara ya kipekee ambayo itasaidia kuimarisha uhusiano wa waumini wa Kanisa Katoliki Duniani hasa ukitilia maanani nchi hiyo ndiyo inawaumini wengi zaidi. Ziara ya Papa Francis nchini Brazil itamchukua kipindi cha juma moja na inatajwa huenda ikawa ni ziara ndefu zaidi ya nje ya Vatican kufanywa na Kiongozi huyo ambaye amekuwa akisisitiza umoja wa waumini wa kanisa hilo

JESHI LA MAREKANI LATOA GHARAMA ZITAZOHITAJIKA KUIVAMIA KIJESHI SYRIA

Jeshi nchini Marekani limeweka hadharani gharama, hatari na faida ambazo zinaweza zikapatikana iwapo nchi hiyo itafanya uvamizi wa kijeshi nchini Syria kwa lengo la kuiangusha Serikali ya Rais Bashar Al Assad inayopambana na Waasi kwa kipindi cha miezi ishirini na nane sasa. Kiongozi wa Juu kwenye Jeshi nchini Marekani Jenerali Martin Dempsey amekiri kuna hatari kubwa na gharama kubwa iwapo nchi hiyo itaivamia kijeshi nchini Syria kitu ambacho kinaweza kikaleta madhara makubwa kwa mustakabali mwema wa baadaye wa nchi hiyo. Jenerali Dempsey ametoa mapendekeo matano ya kijeshi katika kushughulikia mgogoro huo wa Syria akithibitsha udhibiti wa mashambulizi pamoja na kuanzishwa kwa sheria za kuzuia matumizi ya anga la taifa hilo.
Kiongozi huyo wa Kijeshi ameliambia Bunge nchini Marekani kwamba kitendo cha kutumia kikosi cha kijeshi kinaweza kikawa kama vita na huenda vikaleta hasara kubwa kwa taifa hilo na kulazimika kutumia mabilioni ya walipa kodi. Miongoni mwa mambo mengine ambayo amependekeza Jenerali Dempsey yafanyike katika kumaliza umwagaji wa damu nchini Syria ni pamoja na kutoa mafunzo, kushauri na kuwasaidia wapinzani, kuanzisha kambi zao ndani ya Syria pamoja na kudhibiti matumizi ya silaha za kemikali. Jenerali Dempsey amesisitiza kitu muhimu kwa sasa kufanyika ni kuimarisha kikosi cha upinzani kinachopigana na Serikali ya Rais Assad ili kuwe na uwezo wa kupambana ikiwa ni pamoja na kupatiwa zana zaidi.
Haya yanakuja kipindi hiki Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa UN Leila Zerrougui akitoa onyo huenda Viongozi wa Serikali na hata wale wanaopingana na Serikali wakakabiliwa na makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya watoto. Mjumbe huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Watoto ameweka wazi pande zote nchini Syria zimeonekana kufanya uhalifu dhidi ya watoto ikiwemo ni pamoja na kusababisha vifo vya watoto. Mapigano hayo yaliyodumu kwa kipindi cha miezi ishirini na nane yamechangia vifo vya watu zaidi ya laki moja huku wakimbizi wanaokaribia milioni moja na laki nane wakipatiwa hifadhi katika nchi jirani za Jordan na Uturuki.

WATU TISA WAFARIKI KATIKA GHASIA MPYA ZA MISRI

Watu tisa wamepoteza maisha nchini Misri na wengine ishirini na wanane wakijeruhiwa baada ya kuzuka makabiliano makali baina ya wafuasi wa Mohamed Morsi aliyeondolewa madarakani na Jeshi dhidi ya wale wanaompinga kipindi hiki familia yake ikijiandaa kumshtaki Mkuu wa Majeshi Jenerali Abdel Fattah Al Sisi. Mapambano makali yalishuhudiwa katika Mji wa Qalyub wakati ambapo maandamano yaliendelea kushuhudiwa katika Jiji la Cairo kitu kilichochangia Jeshi kuingilia kati kwa ajili ya kurejesha hali ya utulivu wa maeneo hayo. Wafuasi wanaomuunga mkono Morsi ambaye bado anashikilia na Jeshi wamejiapiza kuendelea kufanya maandamano yao kwenye Miji mbalimbali wakiwa na lengo la kushinikiza kurejeshwa madarakani kwa Kiongozi huyo aliyeondolewa na Jeshi.
Ghasia hizo zilishuhudiwa hata katika Wilaya ya Sinai iliyopo Kaskazini mwa Taifa hilo ambapo raia mmoja alipoteza maisha na wanajeshi wanne wamejeruhiwa baada ya kutokea shambulizi lililowalenga. Rais wa Mpito wa Misri Adly Mahmud Mansour ameendelea kutoa wito kwa pande zinazohasimiana kuhakikisha hali ya utulivu inarejea nchini humo ili wananchi washiriki kwenye ujenzi wa taifa kipindi hiki akitaja kikosi ambacho kitakuwa na jukumu la kupitia katiba na kupendekeza mabadiliko. Haya yanakuja baada ya familia ya Morsi kupitia Mtoto wake wa Kike Shaimaa Mohamed Morsi kutangaza nia yao yakumfungulia mashtaka Mkuu wa Majeshi Jenerali Al Sisi kutokana na kuendelea kumshikilia Kiongozi huyo wa zamani.
Shaimaa amewaambia wanahabari watafungua mashtaka hayo kwa kuzingatia sheria za ndani na hata zile za kimataifa kwa kuwa wanaona kinachoendelea kufanywa na Jeshi chini ya Jenerali Al Sisi ni utekeji nyara. Familia ya Morsi imeweka bayana imechoshwa na hatua ya kuendelea kusubiri kuachiwa kwa Kiongozi huyo wa Chama Cha Muslim Brotherhood aliyechanguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kukaa madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee. Mohamed Morsi aliondolewa madarakani tarehe 3 ya mwezi Julai kutokana na kutuhumiwa na maelfu ya wananchi amekuwa akipendelea wafuasi wa Chama Cha Muslim Brotherhood na hivyo maandamano yakaanza kwenye viunga vya Tahrir kushinikiza aondoke madarakani.
Jeshi nchini Misri likaamua kuingilia kati mgogoro huo wa kisiasa na kumtaka Morsi kuzungumza na pande zote kusaka suluhu ya kisiasa kitu ambacho alikikaidi hivyo Jeshi likamuondoa madarakani na kumshikilia sehemu ambayo haijulikani hadi sasa.

JESHI LA KONGO LAZIDI KUPAMBANA NA M23 KWA HELIKOPTA

Jeshi nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC limejigamba kuendelea kushambulia ngome za Kundi la Waasi la M23 zilizopo Mashariki mwa Taifa hilo karibu kabisa na Mji wa Goma wakiotumia helkopta tatu za kijeshi. Taarifa za kijeshi zimeweka bayana helkopta tatu za kijeshi zimeendelea kurusha mabomu kwenye ngome za Kundi la M23 bila ya wapiganaji wa kundi hilo kujibu mashambulizi hayo kitu kinachoashiria wamefanikiwa kuwasambaratisha. Mashambulizi hayo ya Jeshi la Serikali la FARDC kwa kutumia helkopta za kijeshi ni ya kwanza kufanyika mapema leo asubuhi baada ya kuzuka kwa mapigano makali hiyo jana katika Mji wa Kibati na kuchangia maelfu ya wananchi kukimbia makazi yao kueleka Goma. Hofu imeendelea kutanda Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kutokana na kuzuka kwa mapigano mapya kati ya Jeshi la Serikali la FARDC na Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 karibu kabisa na Mji wa Goma na kuchangia maelfu ya wananchi kukimbia makazi yao.
Mapigano hayo yamezuka baada ya kuwepo wa utulivu wa siku nne kitu ambacho kimechangia kuwepo kwa kurushiana kwa maneno baina ya Jeshi la FARDC na Kundi la Waasi la M23 ambapo kila upande umekuwa ukilaumu wenzao kuhusika na kuanzishwa kwa vita hivyo.

Maofisa wa Jeshi la Serikali la FARDC wamethibitisha Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 ndilo lilianza kurusha makombora kulenga kambi zao kitu kilichowasukuma nao kujibu mashambulizi hayo na hivyo kuzuka upya kwa mapigano makali katika Mji wa Kibati.

Msemaji wa Kijeshi wa Kundi la Waasi la M23 Kanali Vianney Kazarama amepeleka lawama kwa Jeshi la FARDC kuwa ndiyo lilianza kurusha mabomu wakitumia ndege za kijeshi kulenga ngome zao kitu kilichowafanya wajibu mashambulizi ili kujihami.

Kanali Kazarama amesema kumekuwa na mapigano makali katika Miji ya Kibati na Uvira lakini Jeshi la Serikali FARDC limeshindwa kuwadhibiti kutokana na wapioganaji wao kuwa imara kukabiliana na mashambulizi yaliyokuwa yanaelekezwa kwao. Mapigano hayo yamezuka umbali wa kilometa nne kutoka Mji wa Goma ambao umekuwa ukisakwa kwa udi nauvumba na Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 kitu kilichochangia maelfu ya wakazi kutoka Kibati kukimbilia mji huo kwa ajili ya kujiepusha na madhara ya vita hivyo. Hakuna taarifa zozote zinazoeleza idadi ya majeruhi au vifo kutoka kwa Jeshi la Serikali FARDC wala Kundi la Waasi la M23 kutokana na mapigano hayo makali yaliyoshuhudiwa katika Miji ya Uvira na Kabati.
Mapema Serikali ya Kinshasa kupitia Msemaji wake na Waziri wa Habari Lambert Mende Omalanga alilinyoshea kidole cha lawama Kundi la Waasi la M23 kwa kutekeleza uhalifu katika Mji wa Kiwanja. Mende amesema taarifa walizonazo zimeonesha Wapiganaji wa Kundi la M23 walivamia nyumba kumi pamoja na kuwapora wanafanyabiashara kumi na tano kabla ya kuua vijana kumi na watatu ma kisha wakabaka wanawake saba na kuwajeruhi wengine kumi na tatu. Jeshi la Serikali la FARDC wamejiapiza kuendelea kuulinda Mji wa Goma kwa gharama yoyote ili kuwazuia Wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23 kuutwaa Mji huo kama walivyofanya awali.

IRAN YAPINGA HIZBULLAH KUINGIZWA KATIKA LIST YA MAGAIDI

Serikali ya Iran imepinga vikali hatua ya Umoja wa Ulaya EU kuliorodhesha Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah katika orodha ndefu ya Makundi ya Kigaidi Duniani wakisema hatua hiyo imechangiwa na shinikizo na kuangalia maslahi ya nchi ya Israel. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Ali Akbar Salehi amelaani uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya EU ambao umepata ushawishi kutoka kwa Taifa hilo la Kiyahudi ambalo limekuwa likishinikiza Kundi la Hezbollah kutambulika kama moja ya makundi ya kigaidi. Salehi amesisitiza kuwa Umoja wa Ulaya EU umekosa pakubwa kwenye uamuzi wake na hilo linachangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na wao kukosa taarifa muhimu juu ya mgogoro unaoendelea kwenye kanda hiyo.
Waziri huyo mwenye dhamana ya masuala ya kigeni katika Serikali ya Tehran amesema Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah tangu lililopokuwa litatambulika kihalali limeweza kuwalinda wananchi wa Lebanon dhidi ya hila za taifa la Israel. Taifa la Iran na Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah wamejiapiza mara zote kuwa Israel ni adui yao na wapo tayari kufanya hata mashambulizi kulilenga Taifa hilo ili waliangamize kitu ambacho kilichangia Serikali Jerusalem kutaka kuwekewa vikwazo kwa Kundi hilo. Serikali ya Iran nimiongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato vya Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah huku pia ikiweka bayana wamekuwa wakitoa msaada wa kijeshi kuhakikisha linaendelea na shughuli zake.
Uamuzi huo wa nchi wanachama ishirini na nane za Umoja wa Ulaya EU umeungwa mkono na Baraza la Taifa la Upinzani nchini Syria ambalo limesema ni sahihi kutokana na Hezbollah kuwa hatari kwenye Ukanda huo. Baraza la Taifa la Upinzani nchini Syria limeweka bayana uamuzi huo wa Umoja wa Ulaya EU usiishie hapo na badala yake Viongozi wa Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah wanapaswa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa vita. Wapinzani nchini Syria wamesema kitendo cha Kundi la Hezbollah kuingilia vita nchini Syria na kulisaidia Jeshi la Rais Bashar Al Assad ni kigezo kingine kuonesha namna ambavyo limekuwa hatari kwa usalama.

M23 WADAI KUWAUWA WANAJESHI 400 WA KONGO

Waasi wa M23 waliojizatiti katika eneo  la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamedai kuwauwa zaidi ya wanajeshi 400 wa serikali ya Kongo  mashariki mwa nchi. Taarifa iliyotolewa leo na waasi hao imeeleza kuwa, tokea yalipoanza mapigano mapya yapata siku 10 zilizopita karibu na mji wa Goma, makao ya jimbo la Kivu Kaskazini, zaidi ya wanajeshi 400 wa serikali ya Kongo wameshauawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kwenye mapigano hayo. Luteni Kanali Vianney Kazarama Msemaji wa waasi wa M23 amesema leo kuwa, wanajeshi hao wa serikali wameuawa katika meneo ya Kibati na Kanyarucinya yaliyoko umbali wa kilomita 15 kutoka mji wa Goma. Wakati  huohuo, raia wasiopungua 10 wamejeruhiwa baada ya helikopta ya jeshi la Kongo kuwashambulia raia kimakosa  mashariki mwa nchi hiyo. Duru za hospitali zinasema kuwa, hali za baadhi ya majeruhi zimeripotiwa kuwa mahututi. Jeshi la Kongo limesema kuwa, shambulio hilo lililenga lilikusudiwa kulenga  ngome ya waasi wa M23 katika eneo la Rumangabo mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, rubani alifanya makosa kwa kuwalenga  raia badala ya waasi.

Saturday, July 20, 2013

SERIKALI YA PYONGYANG YAITAKA PANAMA KUWAACHIA WAFANYAKAZI WA MELI YAKE

Serikali ya Pyongyang imesisitiza kuwa shehena ya silaha zinazozuiliwa na maofisa usalama wa Panama baada ya kuikamata meli yake kuwa ni mpango halali baina ya nchi hizo mbili. Meli ya Korea Kaskazini ilikamatwa kwenye mfereji ewa bahari ya nchi ya Panama, ambapo mara baada ya kufanyiwa ukaguzi ilibainika kuwa Meli hiyo ilikuwa imesheheni silaha zilizotoka nchini Cuba. Awali kabla ya kukamatwa kwa Meli hiyo, maofisa wa Serikali ya Cuba walijaribu kuzuia Meli hiyo isikamatwe lakini walichelewa kwakuwa ilikuwa imeshaingia kwenye himaya ya nchi ya Panama. Ikulu ya Pyongyang hii leo imetoa taarifa kulaani meli yake kushikiliwa pamoja na Sukari ya msaada waliopewa na nchi ya Cuba huku ikitoa wito wa kuachiwa kwa wafanyakazi wa meli hiyo.
Nchi hiyo imeendelea kusisitiza kuwa silaha hizo ni halali na kwamba nyingi ni vifaa ambavyo vingetumika kwenye ukarabati wa silaha nyingine za nchi hiyo ambazo zinahitaji matengenezo. Serikali ya Panama imeandika barua kwa Umoja wa Mataifa UN ikiutaka itume waangalizi wake kwenda nchini humo kubaini iwapo silaha hizo ni sehemu ya zile ambazo nchi ya Korea Kaskazini imewekewa vikwazo. Nchi ya Cuba nayo imeiandikia barua Serikali ya Panama kuitaka iwaachie wafanyakazi wa meli ya Chong pamoja na shehena ya sukari ambayo imekamatwa. Tayari mwendesha mashtaka wa Serikali ya Panama ametangaza kuanza uchunguzi dhidi ya wafanyakazi hao na kwamba iwapo uchunguzi utakamilika watafikishwa mahakamani.

MAANDAMANO MAKUBWA KUPINGA KESI YA ZIMMERMAN

Zaidi ya maandamano 100 yamepangwa nchini Marekani hii leo kwa kile waandalizi wamesema ni kutafuta haki kwa Trayvon kijana mweusi aliyeuawa na George Zimmerman.
Waandamanaji hao wanataka Zimmerman akabiliwe na mashitaka ya ukiukaji wa haki wiki moja baada ya mahakama kutompata na hatia ya kifo cha kijana ambaye hakuwa na silaha Trayvon Martin.Mamake Trayvon na kaka yake wanatarajiwa kushiriki katika maandamano ya Newyork huku babake akishiriki mjini Miami.Kuondolewa kwa mashitaka yote yaliyokuwa yakimkabili Zimmerman na mahakama ya Florida yalizua ghadhabu kote nchini Marekani miongoni mwa wamarekani weusi na kuzua mjadala wa ubaguzi wa rangi.Rais wa Marekani Barrack Obama hapo jana aliizungumzia kesi hiyo kwa mara ya kwanza akisema Trayvon Martin  huenda  angeliweza kuwa yeye miaka 35 iliyopita

MRIPUKO WA BOMU KATIKA UWANJA WA NDEGE BEIJING

Shirika la habari nchini China limesema mtu mmoja ameripua bomu la kutengezwa nyumbani leo katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Beijing katika lango nambari tatu lakini mbali na mshukiwa huyo,hakuna mtu mwengine aliyejeruhiwa katika kisa hicho.
Shrika hilo la Xinhua limewanukuu walioshuhudia wakisema kuwa mripuko ulisikika uwanjani humo saa kumi na mbili na dakika 24 saa za china lakini hawakutoa taarifa zaidi.Kituo cha televisheni cha china Central kimesema katika mtandao wake kuwa mtuhumiwa aliejeruhiwa alikimbizwa hospitali baada ya kuripua bomu hilo na kuongeza kuwa usafiri wa ndege haujaathirika na hali ya kawaida imerejea katika uwanja huo.

LIBYA YAONYA MAKUNDI YA WABEBA SILAHA

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Libya, imeyaonya makundi ya wabeba silaha yanayojihusisha na vitendo vya utekaji nyara nchini humo. Katika taarifa yake iliyoitoa leo, wizara hiyo imeyaonya makundi hayo yanayokwamisha mwenendo wa kisiasa nchini humo na kujihusisha na utekaji nyara wa binaadamu na kuahidi kuwachukulia hatua kali wahusika wa vitendo hivyo. Aidha wizara hiyo imeashiria ongezeko la vitendo hivyo na kusema kuwa, kumekuwepo vitendo vya utekaji nyara huku ikiahidi kuwepo mikakati madhubuti inayoandaliwa kwa minajili ya kukabiliana na hali hiyo. Imesisitiza kuwa, vitendo vya utekaji nyara, vinapingana na uhuru wa binaadamu, na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali ili kuwatia mbaroni wahusika. Hii ni katika hali ambayo, katika wiki kadhaa za hivi karibuni, mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, umekuwa ukishuhudia vitendo vya utekaji nyara na mateso ambavyo hufanywa na watu wenye silaha ambao walipewa ruhusa na wizara hiyo ya mambo ya ndani, kwa ajili ya kuimarisha usalama nchini humo.

HIZBULLAH YAITAKA ISRAEL KUANGALIA MIJI YAKE KABLA YA KUISHAMBULIA LEBANON

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel  katika vita vijavyo  kwanza unapaswa  kufikia hatima ya miji ya utawala huo ghasibu  kabla ya kuishambulia Bairut, na kusisitiza kwamba Israel haina ubavu tena wa kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon. Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, muqawama nchini Lebanon una mitazamo, malengo, majukumu, mikakati  na sera zilizokuwa wazi kabisa. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, utawala wa Israel na nchi zote zilizokuwa nyuma ya utawala huo ghasibu zinaelewa kwamba, si rahisi tena kuishambulia  kijeshi  Lebanon. Sayyid Hassan Nasrullah ameelezea sababu ya kuwa dhaifu jeshi la Lebanon na kusisitiza kuwa, Iran ilitangaza kuwa tayari kulijenga na kuliimarisha jeshi la Lebanon, lakini Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu zilipinga vikali kwa kuhofia kwamba jeshi la Lebanon litakuwa na nguvu zaidi katika eneo.

UFARANSA NA UINGEREZA KUTOWAPA SILAHA WAASI WA SYRIA

Serikali za Uingereza na Ufaransa ambazo kwa miezi kadhaa zimekuwa zikiushinikiza Umoja wa Ulaya kuondoa vikwazo dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Syria, zimefuta mpango wao wa kuwapelekea silaha waasi na magaidi nchini Syria. Duru za habari zinasema kuwa, Uingereza imefikia kwenye natija hii kwamba serikali ya Rais Bashar Assad wa Syria bado ina nguvu na inaweza kuiongoza nchi hiyo kwa miaka kadhaa ijayo, kwa minajili hiyo imeamua kujiondoa kwenye mpango wa kuwapelekea silaha magaidi nchini humo.  Nayo Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ufaransa imetangaza kuwa, Paris hivi sasa haina mpango wa kuwapelekea silaha waasi na magaidi wa Syria. Hivi karibuni makamanda wa kijeshi wa Uingereza walimtahadharisha David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza kwamba, utumwaji siaha dhidi ya magaidi wa Syria unaweza kusababisha hatima mbaya kwa serikali ya London. Makamanda hao wameonya kuwa, silaha hizo watakazopelekewa magaidi huenda zikatumika dhidi ya serikali ya London katika miaka ijayo.

MAREKANI YAISHUTUMU RUSSIA KUTOKANA NA SILAHA ZA KIKEMIKALI

Viongozi wa Russia wamekasirishwa mno na ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani kuhusiana na udhibiti na utokomezaji wa silaha za kemikali. Wizara hiyo imeituhumu Russia kwamba haitekelezi ipasavyo makubaliano ya kuangamiza silaha hizo. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Russia imetoa radiamali kali na kuikosoa Marekani kwamba imetoa taarifa hiyo bila kuzingatia sababu za kimsingi na kwenda kinyume na makubaliano ya kuzuia utumiaji wa silaha za kemikali. Makubaliano ya kuzuia kuzalisha, kutumia na kulimbikiza silaha za kemikali yalifikiwa kutokana na juhudi za miaka kadhaa za jamii ya kimataifa za kuzuia uzalishaji na utumiaji wa silaha hizo  za maangamizi. Taasisi ya Kuzuia Silaha za Kemikali, yenye makao yake mjini The Hague, Uholanzi, ina jukumu la kisheria la kutekeleza makubaliano hayo ya kimataifa. Russia na Marekani ni miongoni mwa nchi wanachama 188 wa taasisi hiyo. Nchi hizo mbili kama ilivyo kwa wanachama wengine, zinapaswa kuangamiza viwanda vyao vya kemikali hatua kwa hatua. Washington na Moscow zinahesabiwa kuwa wamiliki wakubwa wa viwanda vya kemikali duniani na kiwango cha silaha zao za kemikali kinatishia amani ya mabara yote ulimwenguni.  Hadi kufikia mwaka 2010, Marekani ilikuwa imeshatokomeza karibu asilimia 75 ya silaha zake za kemikali. Russia nayo hadi kufikia mwezi Aprili 2012, ilikuwa imeshaharibu asilimia 62 ya silaha hizo. Hata hivyo, Moscow inadai kuwa, hadi kufikia sasa tayari imeshatokomeza asilimia 74 ya silaha zake za kemikali. Kabla ya hapo, Russia iliiomba Taasisi ya Kuzuia Silaha za Kemikali kuiongezea muda wa kutokomeza silaha hizo hadi kufikia mwaka 2015, badala ya muda ulioainishwa awali na taasisi hiyo ya kimataifa wa kuzitaka nchi zote wanachama  kutokomeza silaha zao kufikia mwishoni mwa  mwaka 2012. Aidha Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Russia imeeleza kwenye ripoti yake kwamba, tuhuma kama hizo za Washington zinapoteza hali ya kuaminiana kati ya nchi hizo mbili. Ripoti ya Russia pia imeelezea wasiwasi wake kuhusiana na shughuli za bioteknolojia zinazofanywa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani karibu na mipaka ya Russia. Vyombo vya kidiplomasia vya Russia pia vinaikosoa Marekani kwamba, haitoi fursa kwa Taasisi ya Kuzuia Silaha za Kemikali kufanyika utaratibu wa kusimamia na kupata ripoti za uhakika kutoka kwa nchi wanachama wa taasisi hiyo. Kwa utaratibu huo inaonekana kuwa nchi mbili hizo bado zinaathiriwa na mazingira ya kipindi cha Vita Baridi kwani bado zinahisi hatari kutoka upande wa pili, jambo ambalo linaendelea kuathiri uhusiano wao.

NIGERIA KUTUMA WANAJESHI DARFUR

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa litatuma wanajeshi 800 katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan ili kuisaidia serikali ya Khartoum na kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni humo. Akiwahutubu wanajeshi hao watakaopelekwa huko Darfur, Ahmad Jibrin kamanda wa kikosi cha pili cha jeshi la Nigeria amevitaka vikosi hivyo kuheshimu haki za binadamu na utamaduni wa watu wa Sudan katika muda wote wakataokuweko huko Darfur wakilinda amani. Kamanda huyo wa jeshi la Nigeria amesema kuwa askari wake yoyote atakayetekeleza jinai au uhalifu jimboni Darfur atakabiliwa na hatua kali. Hii ni katika hali ambayo jeshi la Nigeria jana lilitangaza kuwa lina mpango wa kuondoa baadhi ya wanajeshi wake walioko kaskazini mwa Mali baada ya kuboreka hali ya mambo katika eneo hilo na baadaye kuwapeleka wengine.  

BUNGE LA IRAN KUICHUNGUZA BARUA KUHUSIANA NA MAREKANI

Bunge la Iran lapanga  kuchunguza barua ya wajumbe wa bunge la Congress ya Marekani ambayo walimuandikia Rais Barack Obama barua wakitaka afanye mazungumzo na rais-mteule wa Iran Dkt. Hassan Rohani.
Hayo yamedokezwa leo na Alaeddin Boroujerdi Mkuu wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Majlis. Boroujerdi amesema kumekuwepo na ukosefu wa uthabiti katika maamuzi ya Congress kwani bunge hilo hivi karibuni  lilimtaka Obama aiwekee Iran vikwazo vipya na muda mfupi baadaye likamtaka rais huyo wa Marekani afanye mazungumzo na rais-mteule wa Iran.
Hivi karibuni zaidi ya wabunge 131 katika Baraza la Congress walisema kuchaguliwa Dkt. Rohani ni fursa ya kuleta maelewano baina ya Washington na Tehran na hivyo waliitaka Ikulu ya White House itumie njia za kidiplomasia katika kuamiliana na Iran.

SERIKALI YA NDANI YA PALESTINA YASALITI WAPALESTINA

Duru za habari zimetangaza kuwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina imekubali kuendelea na mazungumzo eti ya amani ya Mashariki ya Kati licha ya upinzani wa Wapalestina na sisitizo la Mamlaka hiyo kuwa haitafanya mazungumzo ya aina yoyote na Wazayuni kutokana na ujenzi wake wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina.   Pamoja na kuwa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu makubaliano ya Wapalestina na utawala za Kizayuni kwa ajili ya kuanzisha tena duru mpya ya mazungumzo eti ya mapatano, lakini Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani John Kerry alisema jana usiku baada ya kuhitimisha safari yake ya sita katika eneo la Mashariki ya Kati baada ya kuchukua wadhifa wake huo kuwa, pande husika zitaanza kufuatilia duru mpya ya mazungumzo ya mapatano huko Washington katika wiki ijao.
Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Serikali ya Ndani ya Palestina yalisimama mwezi Oktoba mwaka 2010, wiki nne tu baada ya kuanza huko Washington. Mazungumzo hayo yalisitishwa baada ya utawala wa Kizayuni kukataa kusitisha ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Baitul Muqaddas ya Mashariki. Japokuwa hatua ya Serikali ya Ndani ya Palestina ya kukubali kuanzisha tena duru mpya ya mazungumzo chini ya mashinikizo ya Marekani imekaribishwa na Catherine Ashton, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya na utawala wa Kizayuni, lakini makundi ya Kipalestina hususan harakati ya Hamas, Jihadul Islami na Harakati ya Ukombozi wa Palestina zimepinga kuanza tena mazungumzo hayo eti ya mapatano na kusisitiza kuwa, Mahmoud Abbas hana mamkala ya kuwa msimamizi na mzungumzaji wa masuala muhimu yanayowahusu Wapalestina.  Hii ni kwa sababu kipi cha kisheria cha urais wa Abbas kilimalizika miaka kadhaa iliyopita. Wananchi na makundi ya Kipalestina yanaona kuwa kurejea kwenye meza ya mazungumzo na Israel bila ya kuzingatia maazimio ya Umoja wa Mataifa ni sawa na kuwauwa kisiasa Wapalestina na kutoa mwanya kwa utawala ghasibu wa Israel wa kutenda jinai zaidi dhidi ya Wapalestina.
Wakati huo huo Avigdor Lieberman waziri wa zamani wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni amesema kuwa Tel Aviv kamwe haipo tayari kuanzisha tena mazungumzo ya mapatano na serikali ya Ndani ya Palestina kuhusu mipaka ya mwaka 1967. Lieberman ameyatamka hayo katika radiamali yake kwa habari zilizochapishwa kwamba Israel imekubali kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika fremu ya mipaka iliyoghusubiwa mwaka 1967. Msimamo huo unaonyesha kuwa utawala wa Kizayuni ungali unang'ang'ania takwa lake la kuendelea kughusubu maeneo ya Palestina. Duru mpya ya jitihada za Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani za kufufua mazungumzo eti ya mapatano inakamilika huku raia wengi na makundi ya Kipalestina wakiyataja mazungumzo hayo kuwa yatakuwa na madhara kwa malengo ya muda mrefu ya wananchi wa Palestina.
Alaa kulli hal, kama ilivyosemwa mara kadhaa ni kuwa lengo la safari za kila mara za viongozi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati ni kuzipotosha fikra za walio wengi ili kuficha mipango haramu ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi inayofanywa na utawala wa Kizayuni sambamba na kukanyaga haki za wananchi wa Palestina kupitia mipango hiyo ya urongo.  

MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA BAADA YA SWALA IJUMAA KUPINGA KUPINDULIWA MORSI

Maelfu ya wafuasi wa chama cha Muslim Britherhood wameandamana kwenye miji mbalimbali nchini humo mara baada ya sala ya Ijumaa wakishinikiza kurejeshwa madarakani kwa kiongozi wao, Mohamed Morsi. Maandamano haya ya mara baada ya sala ya Ijumaa yanafanyika wakati ambapo jeshi limeonya dhidi ya kufanyika kwa maandamano ya vurugu na kwamba halitavumilia kuona maandamano hayo yakigeuka kuwa vurugu. Wafuasi hao wa Muslim Brotherhood wameendelea kupuuza tangazo la rais wa mpito, Adly Mansour ambaye amewataka wafuasi hao kuwa watulivu na kuapa kuilinda nchi yake dhidi ya watu wachache wanaotaka kuharibu amani ya nchi.
Maandamano makubwa yameshuhudiwa kwenye eneo la Rabaa al-Adawiya mjini Cairo ambako wafuasi wa Morsi wamepiga kambi toka kiongozi wao alipoondolewa madarakani tarehe 3 ya mwezi July mwaka huu. Viongozi wa Muslim Brotherhood wameyaita maandamano ya hii leo kama ni ya kuvunja mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo na kumrejesha madarakani rais wao Mohamed Morsi. Maandamano haya yanafanyika ikiwa ujumbe wa Umoja wa Ulaya EU uliokuwa nchini humo ukikiri kuwa mzozo huo bado mgumu kuutatua kutokana na pande hizo mbili kutokuwa tayari.
Hapo jana msemaji wa Muslim Brotherhood, Gehad el-Haddad alisema kuwa baada ya kukutana na ujumbe wa EU walitoa mapendekezo yao ya namna ya kusaka suluhu ya kisiasa nchini Misri. Viongozi hao wakaweka wazi nia yao ya kushiriki mazungumzo licha ya kuendelea na msimamo wao wa kutaka Mohamed Morsi arejeshwe madarakani.

Thursday, July 18, 2013

DHAMBI KUBWA YA WANAWAKE WANAOJIFANANISHA KIUME NA WANAUME WANAOJIFANANISHA KIKE.

Mwenyezi Mungu S.W.T. amewalani wanawake wanaojifananisha kiume na wanaume wanaojifananisha kike, na ndio maana ikawa ni katika madhambi makubwa sabini. Mfano wa kujifananisha ni kama vile: Kuzungumza, kutembea, kuvaa mavazi; na kwa wanawake, kumpenda mwanamke mwingine kama wanaume kwa ajili ya kusagana wanawake kwa wanawake (Lesbians), na kwa wanaume, ni kuingiliana wanaume kwa wanaume (Homosexuals). Kutokana na maumbile ya Mwenyezi Mungu S.W.T. ameumba wanaume na ameumba wanawake, na tabia zao na mavazi yao na msemo wao ni tofauti kabisa, lakini ikiwa mwanamume atajifananisha kuwa sawa na mwanamke au mwanamke kuwa sawa na mwanamume, basi watakuwa wamezibadili wao wenyewe taratibu walizopangiwa na kuwekewa na Mola wao, na kwahivyo watakuwa wametenda dhambi kubwa. Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari, “

‘‘لَعَنَ الله الْمُتَشَبِّهَاتِ مِنَ النِّسَاءِ بِالرِّجَالِ وَالْمُتَشَبِّهِينَ مِنَ الرِّجَالِ بِالنِّسَاءِ’’

Maana yake, “Wamelaaniwa na Mwenyezi Mungu wanaojifananisha wanawake kiume na wanaojifananisha wanaume kike.” 
Pia Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi nyingine iliyopokelewa na Ibn Abbaas R.A.A. na kutolewa na Abu Daud, “

‘‘لَعَنَ اللَّه الْمُخَنَّثِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالْمُتَرَجِّلاتِ مِنَ النِّسَاءِ’’

Maana yake, “Mwenyezi Mungu amewalani wanaume wanaojifananisha kike na wanawake wanaojifananisha kiume.” 
Na pia Mtume S.A.W. kasema Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari, “

‘‘لَعَنَ اللَّه المرأة تلبس لبسة الرِّجَالِ والرِّجَالِ يلبس لبسة المرأة’’

Maana yake, “Mwenyezi Mungu amemlani mwanamke anaevaa mavazi ya kiume na mwanamume anaevaa mavazi ya kike.” 

NIGERIA YAKATAA KUMKAMATA AL-BASHIR

Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameondoka nchini Nigeria huku mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC ikitoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi huyo lakini maofisa wa Serikali ya Sudan wamekanusha kiongozi wao kuondoka kwa kuhofia kukamatwa. Suala la kiongozi huyo kuwepo nchini Nigeria lilizua hisia kali toka kwa wanaharakati wa haki za binadamu ambao walikuwa wanaishinikiza Serikali kumkamata kiongozi huyo anasakwa na mahakama ya ICC kwa makosa ya uhalifu wa kivita alioufanya nchini mwake.
Ofisi ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICC ilitoa taarifa kudhibitisha kuwa iliiandikia barua Serikali ya Nigeria kutaka vyombo vya usalama kumkamata kiongozi huyo na kumfikisha kwenye mahakama ya ICC. Hapo jana Serikali ya Nigeria kupitia ikulu ya rais Goodluck Jonathan ilisema haiwezi kumkamata kiongozi huyo kwakuwa hakuja nchini humo kwa mwaliko wa Serikali bali alienda kwa mwaliko wa Umoja wa Afrika ambao walikuwa wameandaa mkutano wa afya kwa viongozi wa bara la Afrika. Hatua ya Nigeria kushindwa kumkamata kiongozi huyo imekosolewa vikali na wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na wanasheria ambao wanadai kuwa Nigeria kama moja ya mataifa yaliyotia saini mkataba wa kutambua mahakama hiyo ilikuwa na wajibu wa kumkamata. Mwaka 2009 na 2010 mahakama ya ICC ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa rais Bashir na viongozi wengine wa Sudan kwa makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu uliofanyika kwenye jimbo la Darfur.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LAAPISHWA MISRI

Rais wa mpito wa Misri ameliapisha baraza lake jipya la mawaziri huku akiwapa nafasi viongozi wenye msimamo wa kati na pia akiwajumuisha wanawake wawili kwenye Serikali mpya. Serikali mpya inaongozwa na waziri mkuu, Hazem el-Beblawi ambaye kwa taaluma ni mchumi, Abdel-Fattah al-Asisi ambaye ataendelea kushikilia nafasi yake ya waziri wa ulinzi na pia Kama naibu waziri mkuu wa kwanza. Waziri wa masuala ya ndani ambaye aliteuliwa na rais aliyepinduliwa, Mohamed Ibrahim ataendelea kushikilia wadhifa wake, huku Nabil Fahmy ambaye aliwahi kuwa balozi wa Misri nchin Marekani, sasa atakuwa Kama waziri wa mambo ya nje. Akisisitiza kwanini baraza lake limejumuisha viongozi wenye msimamo wa Kati, rais wa mpito, Adly Mansour amesema amazingatia mahitaji ya nchi huku akitangaza nafasi tatu za wanawake kwenye baraza lake.
Wizara walizopewa wanawake hao ni pamoja na wizara ya habari, wizara ya afya na wizara ya mazingira, uteuzi ambao unaonekana haukutarajiwa na wananchi wengi. Baraza Hilo jipya lina jumla ya mawaziri thelathini na wanne huku waziri mkuu el-Beblawi akiwajumuisha hajajumuishwa kwakuwa ni waziri mkuu tayari. Hata hivyo baraza hili jipya lililotangazwa na rais Mansour limeonekena kawa la tofauti kutokana na viongozi wengi waliotangulia kujumjisha wanawake wasiozidi wawili kwenye mabaraza Yao. Hata hivyo uteuzi wa mawaziri hao haujajumuisha kiongozi yeyote wa juu toka vyama vya kiislamu huku msemaji wa rais akisema nafasi nyingine wamewekewa viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood. Punde Mara baada ya kutangazwa kwa baraza na kuapishwa, viongozi wa chama cha Muslim Brotherhood wamesema hawatashiriki kwenye Serikali ambayo imeingia madarakani kwa kutumia nguvu za kijeshi na kuapa kufanya maandamano zaidi.
Wafuasi wa Muslim Brotherhood wanalikosoa jeshi la nchi hiyo kwa kuipindua Serikali halali na kuharibu demokrasia ya Misri. Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kawa baraza hilo sio jipya sana kwakuwa karibu mawaziri saba waliokuwa kwenye Serikali iliyoangushwa wameendelea kushikilia nyadhifa zao. Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood, Gehad El-Haddad amelikashifu baraza hilo akisema ni batili na halina mamlaka ya utawala kwakuwa hata Serikali yenyewe haijachaguliwa kidemokrasia.

MWANAHARAKATI WA NDOA ZA JINSIA MOJA AULIWA KIKATILI

Mwanaharakati wa ndoa za watu wa jinsia moja na mwandishi wa habari wa Cameroon, Eric Lembembe ameuawa mjini Yaounde na mwili wake kutelekezwa, mashirika ya kutetea haki za binadamu yamedhibitisha. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na muungano wa mashirika hayo, imesema kuwa shingo na miguu ya mwanaharakati huyo ilikuwa imevunjika huku maeneo ya mkononi na usoni akiwajumuisha amechomwa na pasi. Mpaka sasa sababu ya mauaji yake hazijajulikana licha ya hivi karibuni kabla ya kifo chake kudai kuwa amekuwa akipokea ujumbe wa vitisho toka kwa watu wasiofahamika.  Suala la ushoga na ndoa za watu wa jinsia moja linepigwa marufuku nchini Cameroon na yeyote ambaye anapatikana na hatia ya kitenda kosa hilo anahukumiwa.
Mmoja wa viongozi wa mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Cameroon, Neela Ghoshal amesema polisi hawapaswi kufumbia macho mauaji hayo kwakuwa hata Lembembe mwenyewe alishawahi kuandika maelezo polisi kueleza kupokea vitisho toka kwa watu wasiofahamika. Suala la ndoa za watu wa jinsia moja limepigwa marufuku katika mataifa mengi ya bara la Afrika ambapo wanaopatikana na hatia ya kutenda kosa hilo katika baadhi ya nchi, adhabu yake ni kunyongwa. Mataifa ya magharibi yamejikuta yakiingia kwenye mzozo na mataifa ya Afrika kutokana na baadhi Yao kutishia kusitisha misaada iwapo nchi zao hazitakubakiana na kuruhusu ndoa za watu wa jinsia moja. Ukanda wa Afrika Mashariki ni moja ya maeneo ambayo nchi wanachama haziruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.