Saturday, December 06, 2014

GOOGLE KUTOKA TANZANIA

Wakati nikifanya tafiti zangu za maswala ya shule na kujifunza mambo kadha wa kadha, nikajikuta natafiti juu ya mtandao mkubwa duniani ujulikanao kama "GOOGLE". Imekuwa ni jambo la kawaida kabisa na si la kushangaza kwa wengi pale unapotaja maswala ya kimtandao basi huwezi kukwepa kuutaja mtandao huu. Kwa hapa kwetu Tanzania naweza kuufananisha mtandao huu kama vile zilivyo bidhaa za Bakhresa kwa mkoa wa Dar es salam. Maana kila ukipita basi utakutana na maji, kama si maji basi biskuti, kitoroli cha "ice cream", mkate ama unga wa ngano wenye nembo ya bakhresa. Vile vile, unapokuwa mtandaoni basi ni nadra sana kuukimbia mtandao huu kwani unamiliki makampuni meng kwa wakati mmoja mfano mtandao wa video wa "youtube", google maps, gmail, google drive, google pictures na hata mtandao huu wa "blogspot" unaorahisisha watu kumiliki tovuti basi unamilikiwa na google. 
Mtandao huu umeleta mabadiliko makubwa duniani na bado unaendelea kuleta mafanikio miongoni mwa jamii ya dunia. Lilikuwa ni wazo la wanafunzi wawili tu wa chuo wakati wakisoma na leo ndio viongozi wakuu wa mtandao huu. 
Hivyo basi nirudi kwenye mada kuu, kutokana na mafanikio makubwa ya mtandao huu niliyoyaeleza hapo juu, nimepata kukutana na mawasiliano ya video yaliofanyika kutoka New York, Marekani mpaka katika shule ya msingi ya Katoke iliyopo biharamlo, Tanzania na watu kweza kushuhudia moja kwa moja sehemu nyingine kabisa. Waweza kuitazama video hiyo sasa kwa link hii video