3/11/2012 Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzíbar imetoa taarifa rasmi ya kuruhusiwa kufanya mitihani ya kidato cha
sita, mwezi Februari mwakani, wanafunzi wote 243 wa Zanzíbar waliopewa barua za
kusimamishwa kufanya mitihani hiyo kwa kukosa sifa za kuwa na alama tano.
Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzíbar, Ali
Juma Shamhuna huko Ofisini kwake Mazizini mjini wakati alipokutana na wandishi
wa habari. Waziri Shamhuna amesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo
yake na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Tanzania Bara Dk. Shukuru
Kawambwa yaliyofanyika tarehe 30 Mwezi uliopita mjini Dar es salaam.
Ameseama
kutokana na maamuzi hayo wanafunzi wote waliosajiliwa kufanya mitihani watafanya
mitihani yao baada yamarekebisho ya kasora zilizojitokeza ambazo zilisababishwa
na baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Elimu Bara kujichukulia mamlaka bila
kuijulisha serikali ya Zanzíbar. “Masula ya Elimu ya juu ni masuala ya Muungano,
hivyo maamuzi yake yanapaswa kuwa ya pamaja kwa kushirikisha vyombo husika
ambavyo vipo kwa mujibu wa taratibu na sheria kuwatumikia wananchi wa pande zote
mbili za Tazania.na si vyenginevyo”. alisema Shamuhuna. Alisema maamuzi ya awali
ya kuwasimamisha wanafunzi waliokuwa hawana alama tano, yalitolewa bila ya
kuwepo kikao halali cha Baraza la Mitihani Tanzania NECTA na lililofanyika ni
kuwaandikia barua walimu wakuu wa skuli za Zanzibar jambo ambalo halikupaswa
kutekelezwa kwani vipo vyombo vimewekwa kisheria na taratibu za kufuatwa.
“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Tanzania Bara mweziwe ni Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali ya Zanzbar, ilitakiwa Katibu Mkuu Bara amuandikie
barua rasmi Katibu Mkuu wa Zanzibar kumueleza juu ya mabadiliko yaliyofanyika na
sio kuandikiwa walimu wakuu wa skuli juu ya mabadiliko hayo”.alisema Shamuhuna
Waziri Shamhuna alisema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inawajumbe
wanne katika Baraza la mitihani la Tanzania ambao wao hawajui kupitishwa kwa
maamuzi hayo ispokuwa walikua wakifuata agizo la Serikali ya Mungano. Aliwataja
wajumbe hao kuwa ni Kamishina Baraza la mitihani, Mkurugenzi elimu ya juu,
Mkurugenzi wa Taasisi na lugha za kigeni na mjumbe mwengine kutoka Chuo Kikikuu
cha Taifa Zanzíbar (SUZA). Waziri Shamhuna alisema pamoja na kasoro hiyo
iliyojitokeza bila kutegemewa, Wizara hizo mbili za Elimu za Tanzania Bara na
Zanzíbar kwa muda mrefu zimekuwa zikifanya kazi kwa mashirikino makubwa na
kuleta ufanisi wa hali ya juu.
IMETOLEWA NA IDARA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
IMETOLEWA NA IDARA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO