Saturday, December 15, 2012

MAUAJI YA KINYAMA MAREKANI

Mtu aliyekuwa na silaha nzito amefanya mashambulizi katika  shule ya awali iliyoko katika mji wa Newtown kwenye jimbo la Connecticut, nchini Marekani na kuwaua watu 26 wakiwemo watoto wadogo 20 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 10. Mtu huyo anayekadiriwa kuwa katika umri wa miaka 20, alivamia darasa kwenye shule hiyo ambayo mama yake alikuwa mwalimu na kumfyatulia risasi mama yake pamoja na wanafunzi 18 darasani humo kabla ya kuwauwa watu wazima watano na kisha kujiua mwenyewe. Wanafunzi wengine wawili walifariki wakiwa hospitalini kutokana na majeraha waliyopata. Polisi wamesema kuwa hilo ni moja kati ya matukio mabaya ya mauwaji ya raia katika historia ya Marekani. Polisi imesema kuwa mtu huyo alikutwa amekufa ndani ya shule hiyo. Mtu mwingine alikutwa amekufa kwenye mji huo wa Newtown na kufikisha idadi kuwa 28. Rais Barack Obama ametoa tamko akiwa katika hali ya majonzi makubwa kwenye Ikulu ya nchi hiyo White House na kuapa kupigania udhibiti wa silaha kwa kiwango kikubwa. Muuwaji anaripotiwa alikuwa na silaha nne za mkononi na alivalia mavazi ya kujikinga na risasi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO