Viongozi wa kisiasa nchini Bahrain wameukosoa vikali utawala wa kifalme wa Aal Khalifa kwa kufanya njama dhidi ya wafanya mapinduzi nchini humo. Wapinzani Bahrain wameongeza kuwa, katika kujaribu kuzima wimbi la mwamko wa wananchi utawala wa dhalimu wa ukoo wa Aal Khalifa unatumia mbinu za hadaa na ukandamizaji. Abdullah Al-Gharifi aliyasema hayo hapo jana kupitia televisheni ya Al-Lu'uluat na kusisiza kuwa, katika kuzipotosha fikra za walio wengi na kuyapindisha malengo halali ya Mwamko wa Kiislamu wa wananchi, utawala wa Aal Khalifa umeanzisha wimbi jipya la njama kadhaa. Amesema sasa wananchi wote wamefahamu hila za utawala huo na kwamba, malengo ya mapinduzi yanakaribia. Kiongozi huyo amesisitiza kuwa, pamoja na njama hizo na ukandamizaji unaofanywa na askari wa utawala huo kwa kushirikiana na askari vamizi wa Saudia, bado wananchi wameendelea kusimama imara kwa ajili ya kufikia malengo yao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO