Maelfu ya wanaharakati wa haki za
kuishi nchini Marekani jana Ijumaa wamekusanyika kwenye Mahakama Kuu nchini
humo kupinga uamuzi wa kihistoria wa miaka 40 iliyopita wiki hii ambao
umehalalisha utoaji mimba. Waandaaji wa matembezi ya mwaka kuhamasisha
haki ya kuishi,huko Washington kwenye jengo la taifa la manunuzi,walitarajia
umati mkubwa kupita ule uliojitokeza mwaka jana wa watu wapatao laki nne pamoja
na uwepo wa baridi kali kwa sasa.
Kiongozi wa kanisa katoliki
duniani Papa Benedicto wa 16 ameunga mkono maandamano hayo kwa kutuma ujumbe
mfupi kupitia anwani yake ya mtandao wa twiter akiwatakia kila la heri
wanaharakati hao na kusema kuwa anawaombea viongozi wa kisiasa ili walinde maisha
ya watoto ambao bado hawajazaliwa na kuhamasisha utamaduni wa maisha.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO