Mgombea mwenza katika uchaguzi wa urais kutoka muungano wa CORD Kalonzo Musyoka amedai kwamba kuna udanganyifu unaoendelea katika matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa na tume ya ya uchaguzi IEBC.Musyoka ametoa madai hayo hii leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi.Mgombea huyo mwenza wa waziri mkuu Raila Odinga amesema wana ushahidi kwamba matokeo yanayotangazwa yamefanyiwa mizengwe na kwamba katika baadhi ya vituo idadi ya kura zilizotangazwa ni kubwa zaidi ya idadi jumla ya kura zilizopigwa. Hata hivyo Musyoka ametoa mwito wa utulivu na kusisitiza kwamba madai hayo ya udangayifu sio mwito wa kuingia mitaani kuandamana.Halikadhalika amesema kutokana na yaliyoshuhudiwa mwaka 2007 baada ya kuzuka mvutano juu ya matokeo ya urais , muungano wa Cord unaitaka tume ya uchaguzi kulishughulikia haraka suala hilo kuzuia udanganyifu.Kumekuwa na wasiwasi mkubwa nchini Kenya kutokana na kuharibika kwa mitambo ya elekroniki iliyokuwa ikitegemewa kuendesha shughuli hiyo kwa kasi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO