Monday, December 24, 2012

ANC NAO WAILAANI SERIKALI YA ISRAEL


Chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC kimetoa taarifa rasmi inayolaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na wakati huo huo kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina. Taarifa ya chama hicho imesisitiza kwamba, inaunga mkono jitihada za wananchi wa Palestina za kujiainishia mustakbali wao. Chama tawala cha ANC kimewataka wananchi wa Afrika Kusini kuunga mkono hatua yoyote ile yenye lengo la kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ni hivi karibuni tu ambapo Wabunge wa Afrika Kusini walilaani jinai za Israel na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuushinikiza utawala huo ili usitishe jinai zake dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina. Wapinzani wa Israel nchini Afrika Kusini wanataka kukatwa uhusiano wa kiuchumi na utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO