Monday, December 24, 2012

Wasiwasi wa Ikhwan Muslimin wa Libya


Kundi la Ikhwanul-Muslimin nchini Libya limeeleza wasiwasi wake kutokana na machafuko yanayoendelea huko mwashariki mwa nchi hiyo. Hayo yameelezwa katika ripoti iliyotolewa jana na kundi hilo na kupinga aina yoyote ya machafuko. Kundi hilo pia limesisitiza juu ya udharura wa kulindwa usalama na amani ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Ripoti hiyo imelaani machafuko na mauaji vinavyoendelea nchini Libya na kusisitiza kuwa, taifa la nchi hiyo liko katika hatua muhimu na kwamba pande zote zinatakiwa kulinda umoja wa kitaifa na kuiepusha nchi hiyo na matatizo ya ndani. Imesema kuwa, kuendelea kwa vitendo hivyo vya ukatili, kunayafaidisha mabaki ya utawala uliong’olewa madarakani wa dikteta Muammar Gaddafi.
Katika siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa machafuko na mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi na vikosi vya kulinda amani huko mjini Benghazi mashariki mwa nchi hiyo, ambapo watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO