Thursday, December 13, 2012

MFALME ABDULLAH ARUHUSIWA HOSPITALI

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ameruhusiwa kutoka hospitalini leo, ikiwa ni karibu mwezi moja tangu alipofanyiwa upasuaji wa mgongo. Taarifa iliyotolewa na familia ya kifalme imesema mfalme Abdullah, mwenye umri wa miaka 89 ameondoka kutoka hospitali ya King Abdul Aziz mjini Riyadhi leo mchana. Tarehe 18 Novemba familia hiyo ilitangaza kuwa mfalme Abdullah alifanyiwa upasuaji kurekebisha nyama za juu kwenye mgongo wake na alionekana mara moja tu kwenye luninga tarehe 28 Novemba wakati akipokea wageni katika chumba chake cha hospitalini na tangu wakati huo alikuwa hajaonekana tena. Umri wa mfalme huyo na ugonjwa wa mara kwa mara vimezua wasiwasi juu ya uongozi wa baadaye wa taifa hilo linaloongoza kwa uzalishaji wa mafuta duniani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO