Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania
amesema ifikapo mwaka 2015 hakutakuwa na uhaba wa walimu nchini humo na kwamba
kuanzia mwaka 2020 shule za msingi zitaanza kufundishwa na walimu wenye elimu ya
shahada, kutokana na idadi kubwa ya wahitimu wa fani hiyo watakaokuwa kwenye
soko la ajira. Akizungumza kwenye kongamano linalohusu masuala ya uchumi na
maendeleo lililoandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na
Kitivo cha Uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Kikwete ameongeza kuwa,
katika sekta ya elimu licha ya kuwa na changamoto kadhaa, lakini serikali
imepiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi
wanaoandikishwa kwenye darasa la kwanza, wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu na
vile vya ufundi. Hata hivyo Rais Kikwete amekiri kwamba Tanzania inakabiliwa na
upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, na kwamba jambo hilo linapaswa
kutafutiwa suluhisho.
msamu yauliza inawezekana hii au walimu wenye degree watatafuta kazi nyingine wakafanye.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO