UJERUMANI YAIDHINISHA MPANGO WA PATRIOT
Baraza la mawaziri la Ujerumani limeidhinisha hatua ya kutuma mtambo wa kuzuwia makombora ya kutokea angani, kuilinda Uturuki dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka Syria. Waziri wa Ulinzi Thomas De Maiziere amesema leo kwamba vikosi viwili vya jumla ya wanajeshi 400 vitatumwa katika eneo la mpaka baina ya Uturuki na Syria kwa kipindi cha mwaka mmoja, ijapokuwa muda huo unaweza kupunguzwa. Uamuzi huo sasa unahitaji kuidhinishwa na Bunge la Ujerumani, lakini unaonekana kwamba utapitishwa. Bunge la Uholanzi linatarajiwa kutangaza baadaye leo idhini ya bunge kuhusu hatua kama hiyo. Jumuiya ya Kujihami ya NATO wiki hii ilipitisha ombi la kutuma vifaa vya kuilinda Uturuki dhidi ya mashambulizi ya mpakani kutokea Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO