Marekani imeiwekea Iran vikwazo vipya kwenye sekta ya mafuta, ikiwa ni katika
jitihada mpya za Washington za kutaka kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu
isimamishe shughuli zake za kuzalisha nishati ya nyuklia.
Vikwazo hivyo vilivyoanza kufanya kazi jana vinaizuia Iran kupata
fedha zake za malipo ya mafuta yanayouzwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa vikwazo
hivyo kuanzia sasa fedha zote Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakazopata nje ya
nchi kutoka katika nchi 8 zilizoruhusiwa kununua mafuta ya Iran ikiwemo China,
India na Uturuki zitabakia kwenye akaunti ya Iran nje ya nchi na zinaweza tu
kutumiwa na Iran kununua bidhaa kutoka nchi hizo.
Iran imelaani vikali vikwazo hivyo na kusema kuwa ni hatua nyingine ya
inayoonesha uadui wa Marekani dhidi ya taifa la Iran. Vikwazo hivyo vipya
vimepitishwa siku chache tangu Marekani itangaze kwamba iko tayari kufanya
mazungumzo ya moja kwa moja na Iran.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO