Papa Benedict anafungua akaunti katika mtandao wa kijamii,Twitter, katika jitihada ya kusambaza ujumbe wa kanisa katoliki.
Taarifa kuhusu akaunti hiyo itatolewa baadaye hii leo katika mkutano na waandishi habari, lakini duru kutoka Vatican zinasema huenda asiandike mwenyewe ujumbe kwenye akaunti hiyo. Kanisa hilo la katoliki tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni limezindua mtandao mkuu unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.Wanasema Papa Benedict anapendelea kuandika kwa mkono kuliko kutumia tarakilishi.
Wakatoliki kote duniani, wataweza kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo itakapozinduliwa rasmi.
Papa Benedict anataka kuitumia akaunti hiyo kuwasiliana na wakatoliki kote duniani.
--Hii haimaanishi eti waislam waanze kutumia Mitandao ya kijamii na masheikh wote wawe na twitter ila geuza upande wapili wa na ufikirie kwa umakini zaidi wapi wametoka waislam, wapi walipo na wapi wanakoelekea na JEE DIRA INAFANYA KAZI VIZURI? Chukua hatua
mpaka ilunaga,baswaleh na wenzake waseme ndo watu watazinduka, si unatujua kwa kulalamika lakini utendaji ni ZIRO?
ReplyDelete