Tuesday, December 04, 2012

KWA HILI WAISLAM TUMEJIPANGAJE???

Assalam Alaykum warahmatul lahi wabarakatu. Amma baada ya kumshukuru muumba wa mbingu na ardhi na kumtakia Rehma na Amani kipenzi chake na mtume wetu. Leo hii msamu kama jumuiya inapenda kuongelea juu ya suala la ujenzi wa Campus mpya ya Chuo kikuu cha Afya Muhimbili eneo la mloganzila.

Plan ya ujenzi wa CHUO KIPYA CHA AFYA MUHIMBILI

Katika mbinu za kufanya biashara na kuimarisha dini pia ni kujenga karibu na maeneo ya biashara kama kama walivyofanya waliotutangulia mfano vituo vya mabasi, treni au hata Airport na pia sehemu zinazokusanya watu wengi kwa wakati mmoja kama hospitali, mashule na vinginevyo.Tukirudi katika suala la ujenzi huu kwanza je tumejipanga vipi kuhakikisha kuwa na msikiti ili waislam wenzetu au watoto wetu wataokuja kusoma huko wasije pata taabu wakihitaji kufanya ibada. Tukumbuke kuwa eneo la hospitali ya Muhimbili lililotumika kwa ajili ya msikiti lilikuwa ni wakfu/ swadakatun Jaariya aliyetoa mola amzidishie lakini makafiri nao wakaamua kuanzisha pia eneo lao na kujenga kanisa. Kwa hili waislam hawakufikiria lolote na kwani haikuwa kikwazo kwa wao kuwa na msikiti na sasa chuo kinahama tujiulize


 

1.jee tunaloeneo la kujenga msikiti?

2. makafiri nao jee hawana eneo kweli la kijenga kanisa?

3.kama hakuna eneo, jee kama waislam na watanzania walionunua eneo lolote kwa ajili ya ujenzi wa msikiti karibu na eneo hilo?

4. kama yoote hayo bado nini tunasubiri na nani anahusika zaidi kwa hili?


 

Wenzetu wamejipanga na yaliyonyoyoni mwao ni makubwa zaidi tusitegemee tena eti tukapata tuu hivihivi eneo la kufanyia ibada bila ya kufanya jitihada kwani ni wengi hivi sasa wananunua maeneo ya karibu na eneo hilo ili kufungua anasa mbalimbali na pengine hata ujenzi wa makanisa. Tukija kwa upande wa waislam tunasubiri hadi shekhe fulani atuzindue na tukizinduka kumeshakucha na tunabaki kujilaumu. Hii ni changamoto kwa kila mwenye uwezo na nafasi yake katika kuanzisha harakati za utafutaji wa eneo na hatimaye ujenzi. Tusitegemee tena kuwa na hilo eneo basi kuna sehemu ya msikiti. Mwisho mola shuhudia nimefikisha na aliyesoma amfikishie mwenzake na tuzinduke kabla hayajatufika.


 

..........................wabillahi Tawfiiq.........................

1 comment:

  1. WAISLAM TUNAHAJA YA KULIFUATILIA HILI NA NDUGU MWENYE BLOG TUNASHUKURU KWA KUTUZINDUA ILA NAWE UNAHITAJIKA JUHUDI ZAKO

    ReplyDelete

TUPE MAWAZO YAKO