Thursday, January 10, 2013

IRAN YAZIMA NJAMA ZA KUULIWA WANASAYANSI WAKE


Waziri wa Usalama Iran Sheikh Heidar Moslehi amesema hivi karibuni atatangaza namna maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu walivyozima njama za kuwauwa wanasayansi wa nyuklia nchini.
Akizungumza Jumatano na waandishi habari mjini Tehran, amesema Iran imechukua hatua imara ambazo zimetoa pigo kwa magaidi katika njama zao za kujaribu kuwaua wanasayansi wa nyuklia nchini Iran. Tokea mwaka 2009, wanasayansi wanne wa nyuklia Wairani waliuawa shahidi katika hujuma za kigaidi. Katika hujuma yao ya mwisho, magaidi walimuua shahidi Mostafa Ahmadi Roshan, Januari mwaka jana. Iran imeilaani vikali Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuhusika na mauaji ya wanasayansi wa nyuklia Wairani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO