Monday, March 11, 2013

BENIN NA IRAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WAO

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Benin zimesisitiza juu ya azma zao za kuimarisha na kupanua zaidi ushirikiano baina yao. Hayo yamo katika mazungumzo baina ya Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na Nasiro Bakoo Arifary, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Benin aliyeko safarini hapa mjini Tehran. Rais Ahmadinejad amesisitiza katika mazungumzo hayo kwamba, daima Iran imekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kustawisha uhusiano na nchi zinazojitawala na zinazojitegemea na kwamba, imekuwa ikifuatilia suala hilo kwa nguvu zake zote. Kwa upande wake Nasiro Bakoo Arifary, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Benin amesema nchi yake iko tayari kuimarisha uhusiano na Tehran katika nyanja zote. Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Benin ameisifu misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na masuala mbalimbali ulimwengu na kuzungumzia pia anga ya mazungumzo ya hivi karibuni ya Iran na kundi la 5+1 na kusema kwamba, ana matumaini haki ya Iran ya kustafidi na teknolojia ya kisasa ya nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani itaheshimiwa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO