Sunday, January 13, 2013

JESHI LA ISRAEL LAMUUA MPALESTINA UKINGO WA MAGHARIBI

Jeshi la utawala haramu wa Israel limemuua shahidi Mpalestina katika eneo lenye ukuta wa kibaguzi  huko Ukingo wa Magharibi. Duru zinaarifu kuwa Mpalestina huyo aliyekuwa na umri wa miaka 21 alipigwa risasi Jumamosi kusini mwa mji wa al-Khalil (Hebron) akiwa njiani kuelekea katika eneo lake la kazi.
Hali ya wasi wasi ilitanda katika eneo hilo Ijumaa baada ya wanaharakati wa Kipalestina na kigeni kuweka kambi katika kipande cha ardhi ambacho walowezi wa Kizayuni wamepanga kukipora.  Israel imekaidi matakwa ya kimataifa na kuendeleza ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina. Aidha utawala huo ghasibu wa Israel umekiuka amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ya The Hague na kujenga ukuta wa kibaguzi katika ardhi za Palestina. Israel inakiuka matakwa ya jamii ya kimataifa kutokana na uungaji mkono wa hali na mali kutoka nchi za Magharibi na hasa Marekani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO