Thursday, January 03, 2013

MABEBERU WANAKOSEA KUITATHMINI HIZBULLAH

Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah Sayyid Hassa Nasrullah amesema kuwa, mabeberu wakiongozwa na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni, wanakosea kutathmini uwezo wa harakati hiyo. Amesema wapiganaji shupavu wa Harakati ya Hizbullah hawategemei uwezo wao wa makombora pekee, bali wanategemea imani yao kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad (SAW) na kumpenda na kumuenzi mjukuu wa Mtume Imam Hussein (as). Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyasema hayo leo katika maombolezo ya siku ya Arobaini ya Imam Hussein (as), yaliyofanyika katika mji wa Ba'labak nchini Lebanon. Kwa upande mwingine amezungumzia njama zinazofanywa na mabeberu kwa ajili ya kuzigawa nchi za Kiarabu na kusema, maadui wanapanga njama za kuzigawa nchi za Iraq, Misri, Libya, Syria na Saudi Arabia. Amewataka wananchi wa nchi hizo kutahadhari njama hizo. Aidha amelaani mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wafanyaziara huko nchini Iraq na kusema, vitendo hivyo kamwe havitavunja irada ya ma'ashiki wa Imam Hussein (as) na kwamba kila mwaka wafanyaziara watakuwa wakimzuru mjukuu huyo wa Mtume (SAW), bila ya khofu yoyote. Kuhusu Syria kiongozi huyo wa Hizbullah amesema kuwa, njia pekee ya kumaliza mgogoro wa nchi hiyo ni kupitia mazungumzo ya kitaifa na kwamba, taifa hilo litageuka na kuwa lenye nguvu na uwezo mkubwa katika eneo hili.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO