Wednesday, January 02, 2013
SUDAN KUSINI TUKO TAYARI KUONDOA MAJESHI MPAKANI
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema kuwa nchi yake iko tayari kuondoa wanajeshi wake katika mpaka unaogombaniwa kati ya nchi hiyo na Sudan. Rais wa Sudan Kusini ameyatamka hayo katika hotuba yake ya kuukaribisha mwaka mpya na kuongeza kuwa yeye na mwenzake wa Sudan Omar al Basher wamepanga kukutana baadae mwezi huu katika juhudi za kutafuta njia ya kuainisha eneo la mpaka ambalo litasimamiwa na wanajeshi wa nchi zote mbili na wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa. Amesema Juba imeamua kuondoa wanajeshi wake kwa muda katika eneo la mpaka lenye mzozo kati ya Sudan Kusini na Sudan ili kuweza kuanzisha kikosi cha wanajeshi watakaosimamia eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO