Friday, January 04, 2013

VIONGOZI WA SUDAN MBILI WAKUTANA


Viongozi wa nchi mbili hasimu za Sudan na Sudan Kusini wanakutana leo katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa kwa ajili ya kuhuisha makubaliano yaliyokwama kuhusu masuala ya uchumi, mafuta na ulinzi. Mazungumzo ya leo kati ya Rais Omar Hassan Albashir na mwenzake wa Sudan Kusini, Salva Kiir yatafanyika baada ya jeshi la serikali ya Juba kuituhumu Khartoum kwamba imeanzisha mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya Sudan Kusini.
Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Philip Aguer amesema kuwa jeshi la Sudan limevamia ardhi ya Sudan Kusini huku ndege za kijeshi zikiendelea kurusha mabomu katika vijiji vya eneo la Raja katika jimbo la Bahr el-Ghazal. Amesema kuwa mapigano hayo yalikuwa yakiendelea hadi jana jioni na kwamba idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa bado haijajulikana.Madai hayo hayajathibitishwa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wala chombo chochote kile huru.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO