Friday, January 04, 2013

UMASIKINI NA NJAA VYAONGEZEKA MAREKANI


Idadi ya watu maskini na wasio na makazi inazidi kuongeza nchini Marekani. Ripoti zinasema kuwa licha ya Kongresi ya Marekani kupasisha mpango wa kuiepusha nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro wa kifedha na sheria hiyo kutiwa saini na Rais Barack Obama, lakini hatua hizo si suluhisho la mgogoro wa madeni ya serikali ya Washington na umasikini unaoongezeka siku baada ya siku nchini humo.
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umetangaza kuwa mpango wa kuiepusha Marekani kutumbukia katika mgogoro mkubwa wa kifedha uliopasishwa siku chache zilizopita si suluhisho la matatizo ya muda mrefu ya nakisi ya bajeti na madeni makubwa ya serikali ya nchi hiyo.
Taasisi inayotathmini viwango vya uchumi ya Moody's imekariri wasiwasi wa shirika la IMF kuhusu uchumi wa Marekani na kutangaza kuwa hatua zilizochukuliwa haziwezi kutatua matatizo ya nakisi ya bajeti ya nchi hiyo kwa kipindi kifupi.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni zinaonesha kuwa idadi ya watu wasio na makazi katika miji 25 mikubwa ya Marekani imeongezeka kwa asilimia 7 tangu mwaka 2011 na kwamba mishahara midogo na gharama kubwa za maisha vimechangia katika ongezeko la watu wanaosumbuliwa na njaa nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO