Msemaji wa White House Jay Carney amesema kuwa, Marekani itaongeza misaada
kwa waasi wanaopigana na serikali ya Syria eti kwa lengo la kuharakisha
mabadiliko ya kisiasa katika nchi hiyo.
Matamshi hayo yametolewa huku gazeti la Washington Post likiandika kuwa,
White House inaazimia kuwatumia waasi wa Syria silaha, magari ya kijeshi na
ikiwezekana pia kuwapatia mafunzo ya kijeshi. Marekani imekuwa ikiwafadhili
waasi wa Syria kwa lengo la kumuondoa madarakani Rais Bashar al Assad wa nchi
hiyo.
Katika upande mwingine mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amewataka
wanaojiita 'Marafiki wa Syria' kuwashauri wapinzani kukaa kwenye meza ya
mazungumzo ya kitaifa na serikali bila masharti. Bashar al Jaafar amesema, iwapo
kweli watu hao ni marafiki wa kweli wa taifa la Syria na wanajali wananchi wa
nchi hiyo wanapaswa kuwashauri wapinzani kufanya mazungumzo ya kusitisha
mapigano na kutoharibu zaidi miundombinu ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO