WEPESI WA KUHIFADHI QUR-AAN
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“Na kwa yakini Tumeifanya Qur-aan iwe nyepesi kufahamika (ili iwe kikumbusho). Lakini yuko anayekumbuka?” Al-Qamar: 17
Yaani tumemfanyia wepesi katika kuhifadhi je yupo anayeelekea akatafuta kuhifadhi akasaidiwa - Tafsiyr Al-Qurtubiy
Mtoto mdogo chini ya miaka kumi ameweza kuhifadhi Qur-aan yote pia asiyejua Lugha ya Kiarabu ameweza kuhifadhi na haya yashatokea.
KUHIFADHI QUR-AAN HAINA UMRI MAALUM
Wanadhani watu wengi kwamba kuhifadhi Qur-aan ina wakati maalum katika maisha ya mwanaadamu nayo ni kipindi cha udogoni wanarudiarudia methali mashuhuri “kuhifadhi udogoni ni kama nakshi katika jiwe” na wanatolea dalili pia kwamba kipindi cha ukubwa inashughulika akili kwa mambo ya kimaisha.
Maneno haya yanahitaji yatizamwe upya, ni kweli kuhifadhi udogoni ina faida zake lakini haiishii hapo, mwanaadamu Akiwezeshwa na Allaah akajitahidi na kufanya subra anaweza kwa uwezo wa Allaah kulifikia hilo hata katika umri mkubwa.
Yaani tumemfanyia wepesi katika kuhifadhi je yupo anayeelekea akatafuta kuhifadhi akasaidiwa - Tafsiyr Al-Qurtubiy
Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) ilikuwa Qur-aan inawashukia wakaihifadhi vifuani mwao na hawakuwa katika umri wa utoto mfano Makhalifa wanne, Ubay bin Ka’ab, Zayd bin Thaabit, Ibn Mas’uud na wengineo.
Imekuja kutoka kwa Ibn Mas’uud kwamba amesema, “Alifariki Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam) nami nina miaka kumi na nimeshasoma al-Muhkam na al-Mufaswal (yaani kuanzia Surat Al-Hujuraat mpaka An-Naas). Al-Bukhaariy
Maana yake alikamilisha kuhifadhi Qur-aan baada ya hapo kama Ubay bin Ka’ab na Zayd bin Thaabit.
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alihifadhi Suratul Baqarah kwa miaka kumi na alipomaliza alichinja Ngamia kumshukuru Allaah na hii ni dalili kwamba kuhifadhi haina umri maalum wala wakati maalum.
NJIA KUMI ZA KUHIFADHI QUR-AAN
1. HATUA YA KWANZA
IKHLAAS NA NIA YA KWELI
Qur-aan ni maneno ya Allaah na kheri ya maneno, Naye hampi hii zawadi na fadhla (ya kuhifadhi) ila kwa aliyemjua ukweli wa nia yake na ikhlaas kwake Yeye. Na mwanaadamu bila ya nia ya kweli na ikhlaas inakuwa kazi yake ni bure.
Anasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam):
“Kila tendo ni kwa niyah na kila mtu atalipwa kwa niyah yake.” Al-Bukhaariy
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasema:
“Mwenye kujifundisha elimu inayotakiwa kwa ajili ya radhi ya Allaah akaitafuta ili apate cheo cha kidunia hatopata harufu ya pepo.” At-Tirmidhiy
Tunamuomba Allaah Atutengenezee niyah zetu na matendo yetu na Ajaalie tufanye kwa ajili Yake.
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) anasema:
Tunamuomba Allaah Atutengenezee niyah zetu na matendo yetu na Ajaalie tufanye kwa ajili Yake.
itaendelea Ijumaa ijayo insha-Allah...........
Sasa Part 1,mbona Siioni,naona tu itaendelea wiki ijayo,ya wiki iliyopita iko wapi.
ReplyDelete