Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajitayarisha kuiondolea Somalia
vikwazo vya silaha ambavyo vimekuwa vikitekelezwa kwa miongo miwili sasa. Duru za kidiplomasia zinasema uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa unalenga
kuisaidia serikali ya Somalia iweze kukabiliana na waasi hasa wanamgambo wa Al
Shabaab ambao bado wanaendelea kutekeleza mashambulizi nchini humo.
Imearifiwa kuwa katika kikao chake cha wiki ijayo, Baraza la Usalama
litaidhinisha kuongezea muda wa Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Afrika
Somalia AMISOM pamoja na kuiondolea Somalia vikwazo vya silaha. Baraza la
Usalama liliiwekea Somalia vikwazo vya silaha mwaka 1992 wakati wababe wa kivita
walipoanza kuwania madaraka baada ya kuangushwa utawala wa Mohammad Siad Barre.
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia aliyechaguliwa mwaka jana amekuwa
akitembelea nchi za Magharibi akitaka vikwazo vya silaha dhidi ya nchi yake
viondolewe.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO