Tuesday, March 05, 2013

ISRAEL YAONYA BARAZA LA USALAMA JUU YA SYRIA

Israel imelionya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana, kuwa haitokaa na kuangalia tu wakati vita vya Syria vikisambaa ndani ya mipaka yake. Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Ron Prosor, ameliandikia Baraza hilo lenye wanachama 15, kulalamika juu ya makombora yanayotua nchini mwake kutoka Syria. Alisema nchi hiyo isitarajiwe kunyamaza wakati maisha ya raia wake yakiwekwa hatarini na vitendo vya kizembe vya serikali ya Syria. Kwa upande wake, Balozi wa Urusi katika Umoja huo, Vitaly Churkin, ambaye ndie rais wa Baraza kwa mwezi wa Machi, amesema usalama wa Israel na Syria ulikuwa unatishiwa pia na kuwepo kwa makundi yenye silaha yanayoendesha shughuli zake katika eneo linaloyaunganisha mataifa hayo katika milima ya Golani, ambalo lilitekwa na Israel wakati wa vita vya mwaka 1967. Eneo hilo haliruhusiwi kuwa na shughuli za kijeshi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO