Tuesday, March 05, 2013

MISRI YALAANI MATUKIO YA ASKARI WA ISRAEL HUKO AL-AQSA


Chuo Kikuu cha Kidini cha al Azhar nchini Misri kimezitaka taasisi za kimataifa na wapenda haki duniani  kuchukua hatua kali dhidi ya askari wa utawala wa Israel aliyepiga teke kitabu cha Qurani Tukufu na kuwanajisi wanawake kadhaa waliokuwa wakihifadhi Qurani Tukufu ndani ya Msikiti wa al Aqswa.
Taarifa iliyotolewa na Chuo Kikuu cha al Azhar imelaani vikali kitendo cha askari huyo wa Kizayuni cha kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, tukio hilo ni sehemu ya mlolongo wa jinai zinazofanywa na Wazayuni  dhidi ya Quds Tukufu, matukufu ya Kiislamu na dhidi ya wakaazi wa eneo hilo, huku jamii ya kimataifa ikifumbia macho vitendo hivyo.
Taarifa hiyo imeutaka umma wa Kiislamu, Kiarabu na wapenda haki duniani kuchukua hatua kali za kukabiliana na kitendo hicho cha kuivunjia heshima Qurani Tukufu  na kile cha kunajisiwa wanawake wa Kiislamu wa Kipalestina. Aidha al Azhar imezitaka taasisi za kimataifa kuweka sheria za kuadhibiwa wale wote watakaopatikana na kosa la kuyavunjia heshima matukufu ya dini za mbinguni na matukufu ya wafuasi wa dini hizo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO