Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri amemtimua kazi Meja Jenerali Majid Nouh Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia nchini humo. Meja Jenerali Muhammad Ibrahim al Juma'a amemtimua kazi Meja Jenerali Majid Nouh na badala yake amemteua Meja Jenerali Ashraf Abdullah kuziba nafasi hiyo. Siku ya Alhamisi iliyopita, mamia ya polisi wa Misri walifanya mgomo na kutaka aondolewe Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo. Polisi wa Misri wanamtuhumu waziri huyo kuwa alitumia kikosi cha usalama kwa shabaha ya kufikia malengo yake ya kisiasa. Kwa upande mwengine, jeshi la polisi katika mji wa Port Said nchini Misri limekabidhi ulinzi wa usalama wa mji huo kwa jeshi la nchi hiyo ili kukabiliana na ghasia na machafuko ya barabarani yanayoendelea mjini humo kwa siku kadhaa sasa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO