Saturday, March 09, 2013

WAZIRI WA MISRI ASISITIZA KUREJESHA UTULIVU


Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imesema kuwa vikosi vyake vyote viko tayari kurejesha amani na utulivu nchini humo. Wizara hiyo imetangaza kuwa vikosi vyote, wakiwemo wanajeshi na polisi wa wizara hiyo wako tayari kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama nchini na kujitolea kwa lolote.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imesisitiza pia juu ya uungaji mkono wa wananchi kwa makundi yote ya kimapinduzi, kisiasa na kimichezo ya nchi hiyo na kuyataka makundi hayo kuwasilisha maoni na matakwa yao kwa kufuata misingi ya kidemkorasia katika kipindi nyeti cha hivi sasa.  Wizara hiyo imeongeza kuwa mchafuko yaliyoikumba nchi hiyo hivi karibuni yanatishia maslahi ya wananchi na taasisi za umma na binafsi za nchi hiyo. Imesema kuwa inaheshimu na kufungamana na majukumu yake yote kwa mujibu wa katiba ili kuzuia kuenea machafuko katika pembe mbalimbali za Misri. Mji mkuu wa Misri Cairo na khususan maidani ya at-Tahrir na maeneo ya karibu na balozi za Marekani na Uingereza mjini humo hivi karibuni yalishuhudia mapigano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji, na kupelekea watu kadhaa kujeruhiwa. Alhamisi iliyopita mji wa Port Said pia ulikumbukwa na mapigano kati ya vikosi vya usalama na wafanya maandamano ambapo watu 471 walijeruhiwa.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO