Thursday, March 07, 2013

WAKOREA WATISHIANA UBABE

Jeshi la Korea Kusini limesema iwapo Korea Kaskazini itaanzisha mashambulizi dhidi yake, litajibu mapigo tena kwa kishindo kikubwa. Jeshi hilo limesema litawalenga viongozi wakuu wa Pyongyang kama njia ya ulipizaji kisasi kwa shambulio lolote. Hii ni katika hali ambayo, Korea Kaskazini imetishia kujiondoa kwenye mkataba wa usitishaji vita kati yake na jirani yake Korea Kusini iwapo Seoul na Washington zitaendelea na mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika peninsula ya Korea. Mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini yalianza Machi 1 na Korea Kaskazini imesema yanatishia usalama wa wananchi wake. Korea mbili zilitiliana saini makubaliano ya usitishaji vita mwaka 1953 na hivyo kuhitimisha vita vya miaka mitatu kati yao. Korea Kaskazini imeipa Korea Kusini hadi Machi 11 isimamishe mazoezi ya pamoja ya kijeshi na Marekani la sivyo ijiondoe kwenye makubaliano hayo.
Kwa upande mwingine Jeshi la Korea Kusini limesema kwamba litaishambulia Korea Kaskazini na kuwalenga viongozi wake ikiwa serikali hiyo ya Korea Kaskazini mjini Pyongyang itafanya mashambulizi iliyotishia kuyafanya kujibu hatua inazoziita za uchokozi za Marekani na Korea Kusini.Wanajeshi wa Korea Kusini na Marekani walifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi hatua ambayo imeikasirisha Korea Kaskazini.Hapo jana mmoja kati ya majenerakli wakuu wa Korea kaskazini alijitokeza katika tukio la aina yake kwenye televuisheni na kusema kwamba serikali ya Pyongyang imefutilia mbali makubaliano yake ya kuacha shughuli za kijeshi na Marekani na kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Marekani na Korea Kusini ikiwa nchi hizo zitaendelea na mazoezi yao ya pamoja ya kijeshi yaliyoanza Marchi mosi.Mvutano na wasiwasi umeongezeak kati ya korea hizo mbili tangu upande wa kaskazini ulioko chini ya utawala wa Kim Jong un aliyeingia madarakani takriban mwaka mmoja uliopita  kufanya majaribio ya roketi la masafa marefu mwezi Desemba uliopita.Hatua hiyo ya Korea Kaskazini ilichochea Umoja wa Mataifa kupitisha vikwazo zaidi dhidi ya taifa hilo ambavyo vinatarajiwa kutangazwa rasmi siku ya Alhamis baada ya Marekani na China mshirika wa Korea Kaskazini kufikia makubaliano ya kuiadhibu serikali ya Pyongyang.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO