Makamu wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema maadui wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hugo Chavez walimpa sumu ya saratani ambayo imepelekea aage dunia baada ya kuugua kwa miaka miwili. Maduro ameyasema hayo sambamba na kuwatimua maafisa wawili wa Jeshi la Anga la Marekani nchini humo ambao walikamatwa wakifanya ujasusi jeshini na kupanga njama za kuvuruga amani nchini humo. Maafisa wa serikali ya Venezuela wameinyoshea kidole Marekani na kusema ndio mhusika mkuu katika kupewa sumu Chavez.
Rais Hugo Chavez wa Venezuela alifariki dunia jana Jumanne baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda wa miaka miwili. Nicolas Maduro Makamu wa Rais wa Venezuela alitangaza habari ya kifo cha Rais Chavez jana jioni kupitia televisheni ya taifa.
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwenye ujumbe wake wa rambirambi kwamba, mwenzake Chavez atabakia kuwa nembo ya harakati dhidi ya ubeberu duniani. Rais wa Iran amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Chavez na kuongeza kuwa, wananchi na viongozi wa Iran wako pamoja na wenzao wa Venezuela katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO