Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya
Lebanon imekanusha madai kuwa imetuma ndege isiyokuwa na rubani (drone) katika
ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina huko Israel. Jeshi la utawala haramu
wa Kizayuni jana lilitangaza kuwa, limetungua ndege isiyo na rubani inayodaiwa
kumilikiwa na harakati ya Hizbullah ya Lebanon karibu na bandari ya kaskazini
mwa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Msemaji wa Jeshi la
utawala huo alisema kuwa, ndege hiyo ilitambuliwa ikiwa katika anga ya Lebanon
katika umbali wa kilometa nane kutoka pwani ya magharibi mwa Haifa na
kudondoshwa na jeshi la Israel.
Katika upande mwingine Waziri wa Mambo ya Nje wa
Lebanon amesema kuwa harakati ya Hizbullah haiingilii masuala ya Syria. Adnan
Mansour amesema kwamba, askari wa Hizbullah wapo kwenye vijiji vya mpaka wa
Lebanon kwa ajili ya kulinda Walebanoni wa eneo hilo na wala hawashiriki katika
operesheni za kijeshi ndani ya Syria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO