Wapiganaji wa kiislamu wa Syria na Iraq watangaza dola ya kiislamu yaani Khilafa ikimaanisha mrejesho wa utawala huo uliomalizika takribani miaka 100 iliyopita baada ya kuanguka kwa utawala wa Ottoman. Kutokana na sauti zilizohifadhiwa na kusambazwa mtandaoni jumapili hii, utawala wa kiislamu wa Iraq na ISIL wamethibitisha kuwa Kiongozi wao Abu Bakr Al-baghdadi kuwa ndio Khalifa wao na ndio kiongozi wa waislamu wa kila mahali. Baghdadi anaaminika kuwa kiongozi wa ISIL, ambayo ilijitangaza rasmi kuwa ni Taifa la kiislamu. Kutokana na maelezo yao, utawala huo mpya unaanzia nchini Iraq katika jimbo la Diyala mpaka Aleppo nchini Syria.
''Shura ya utawala wa kiislamu ilikutana na kujadili kuhusiana na utawala wa kiislamu. Hivyo utawala wa kiislamu uliamua kuanzisha khilafa na kumchagua khalifa wa waislamu wote'' aliarifu msemaji wa ISIL Abu Mohammad Al-Adnani.
''Majina ya 'Iraq' na 'the Levant' yameondolewa katika orodha ya taarifa muhimu ya utawala huo wa kiislamu'' alisema Adinani, akielezea kuwa utawala wa kiislam 'khilafa' ni ndoto ya waislamu wote na ni tumaini la wana-jihad wote. Inadhaniwa kuwa tangazo hilo linaweza kuleta mtafaruku kwa wapiganaji wengine wa kisunni nchini Iraq ambao wanapigana na serikali ya waziri mkuu Nour Al-Maliki na sio wanaopigana kwa ajili ya khilafa.
Chanzo: www.mwcnews.net
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO