Wednesday, April 24, 2013

KENYATTA AANZA KUUNDA SERIKALI YAKE


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya ambapo ametangaza majina ya mawaziri wanne. Wanne hao ni pamoja na Dkt. Fred Okeng'o Matiangi ambaye ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa wizara ya Fedha, James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na Balozi Amina Mohammed ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.
Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja mawaziri wote 18, lakini amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba taifa kuwa na subira. Huku haya yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha kamati maalum ambayo itawachuja mawaziri watakaoteuliwa na Rais. kamati hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.
Chini ya katiba ya Kenya sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO