Iran na Russia zimetoa wito wa kufanyika
mazungumzo bila masharti kama njia ya kuhitimisha mgogoro wa Syria uliopelekea
maelfu ya watu kuuawa katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa. Wito huo
umetolewa katika mazungumzo kati ya Hussein Amir Abdollahian Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje wa Iran na mwenzake wa Russia Mikhail Bogdanov yaliyofanyika hapa
mjini Tehran. Wawili hao walijadili pia njia za kusaidia pande za Syria
kuanzisha mchakato wa kisiasa utakaoweza kusaidia kuhitimisha mapigano nchini
humo.
Katika upande mwingine jeshi la Syria limedhibiti
mji muhimu karibu na Damascus baada ya wiki kadhaa za mapigano na waasi
wanaofadhiliwa kwa fedha na silaha na nchi za kigeni. Mji huo wa kistratejia wa
Otaybah umedhibitiwa na jeshi la Syria baada ya mapigano makali yaliyopelekea
waasi wengi kuuawa. Mji huo ulikuwa unatumiwa na waasi kupitishia s
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO