Maelfu ya raia wa Nigeria wamekimbilia nchini Cameroon wakihofia usalama wa maisha yao baada ya jeshi la nchi hiyo kuanzisha operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya kundi la Boko Haram. Taarifa zaidi zinasema kuwa, maelfu ya raia hao wamewasili nchini Cameroon baada ya jeshi la serikali ya Nigeria kufanya mashambulio makubwa katika ngombe za Boko Haram na baadhi ya vijiji vya kaskazini mwa Cameroon. Taarifa zaidi zinasema kuwa, mamia ya raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto jana walikimbia vijiji vyao na kukimbilia katika maeneo ya mpakani na Cameroon. Wakati huo huo jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limewatia mbaroni watu 120 wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa duru za kijeshi, wanachama hao wa Boko Haram walitiwa mbaroni huko Maiduguri wakati walipokuwa wakishiriki katika mazishi ya mmoja wa kamanda wao aliyeuawa hivi karibuni katika operesheni ya kijeshi ya vikosi vya serikali. Hayo yanajiri katika hali ambayo, jeshi la Nigeria limesema kwamba wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wamedhoofika na kwamba wanaikimbia nchi hiyo kwa idadi kubwa baada ya kushambuliwa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO