Wednesday, June 19, 2013

MABOMU YA NYUKLIA YA US YAMEHIFADHIWA UHOLANZI

Ruud Lubbers, waziri mkuu wa zamani wa Uholanzi ameeleza kuwa mabomu ya nyuklia 22 ya Marekani yamehifadhiwa katika kituo cha jeshi la anga nchini humo. Lubbers amethibitisha kuwa mabomu hayo ya nyuklia ya Marekani yamekuwa yakihifadhiwa katika vyumba imara chini ya ardhi huko kwenye kituo cha kijeshi cha jeshi la anga cha Brabant. Ruud Lubbers aliyekuwa waziri mkuu wa Uholanzi kuanzia mwaka 1982 hadi 1984 ni afisa wa kwanza wa ngazi ya juu wa Uholanzi kukiri kuweko mabomu ya nyuklia katika ardhi ya nchi hiyo. Mabomu hayo ya nyuklia ya Marekani yametajwa kuwa ni aina ya B61 yaliyozalishwa nchini Marekani katika muongo wa 60 na kwamba yana nguvu mara nne zaidi ya yale yaliyotumiwa katika miji ya Japan ya Hiroshima na Nagasaki wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO