Wanajeshi watatu wa Jumuia ya Kujihami ya NATO,wameuwawa nchini Afghanistan.Msemaji wa vikosi vya kimataifa vinavyoongozwa na jumuia ya NATO nchini Afghanistan-ISAF amesema wanajeshi hao wameuwawa katika mashambulio tofauti yaliyojiri kusini na mashariki ya nchi hiyo.Hajasema lakini wanajeshi hao ni raia wa nchi gani. Wanajeshi wa Kimarekani wanasemekana wako kwa wingi katika eneo hilo.Kwa mujibu wa duru za ISAF, raia mmoja pia ameuwawa kufuatia mashambulio hayo.Mashambulio dhidi ya vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini Afghanistan yamezidi kuongezeka.Jumuia ya kujihami ya NATO imepanga kuwaondowa wanajeshi wake kutoka Afghanistan hadi ifikapo mwisho wa mwaka 2014 .
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO