Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel katika vita vijavyo kwanza unapaswa kufikia hatima ya miji ya utawala huo ghasibu kabla ya kuishambulia Bairut, na kusisitiza kwamba Israel haina ubavu tena wa kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon. Sayyid Hassan Nasrullah amesisitiza kuwa, muqawama nchini Lebanon una mitazamo, malengo, majukumu, mikakati na sera zilizokuwa wazi kabisa. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, utawala wa Israel na nchi zote zilizokuwa nyuma ya utawala huo ghasibu zinaelewa kwamba, si rahisi tena kuishambulia kijeshi Lebanon. Sayyid Hassan Nasrullah ameelezea sababu ya kuwa dhaifu jeshi la Lebanon na kusisitiza kuwa, Iran ilitangaza kuwa tayari kulijenga na kuliimarisha jeshi la Lebanon, lakini Marekani na baadhi ya nchi za Kiarabu zilipinga vikali kwa kuhofia kwamba jeshi la Lebanon litakuwa na nguvu zaidi katika eneo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO