Serikali za Uingereza na Ufaransa ambazo kwa miezi kadhaa zimekuwa zikiushinikiza Umoja wa Ulaya kuondoa vikwazo dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Syria, zimefuta mpango wao wa kuwapelekea silaha waasi na magaidi nchini Syria. Duru za habari zinasema kuwa, Uingereza imefikia kwenye natija hii kwamba serikali ya Rais Bashar Assad wa Syria bado ina nguvu na inaweza kuiongoza nchi hiyo kwa miaka kadhaa ijayo, kwa minajili hiyo imeamua kujiondoa kwenye mpango wa kuwapelekea silaha magaidi nchini humo. Nayo Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ufaransa imetangaza kuwa, Paris hivi sasa haina mpango wa kuwapelekea silaha waasi na magaidi wa Syria. Hivi karibuni makamanda wa kijeshi wa Uingereza walimtahadharisha David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza kwamba, utumwaji siaha dhidi ya magaidi wa Syria unaweza kusababisha hatima mbaya kwa serikali ya London. Makamanda hao wameonya kuwa, silaha hizo watakazopelekewa magaidi huenda zikatumika dhidi ya serikali ya London katika miaka ijayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO