Inna Lillahi Wainna Ilayhi Raajiuun...........Nahid Almanea alikuwa ni mwanafunzi wa shahada ya pili kutokea Saudi Arabia wakati akiuwawa katika mashambulizi mabaya wiki iliyopita huko Colechestor, Essex nchini Uingereza. Msichana huyu alichomwa na kitu chenje ncha kali mara 16 katika mwili wake wakati akipita katika mitaa ya jiji hilo. Polisi bado wanaendelea na msako wa waliohusika na mashambulizi hayo. Tayari dada huyu ameshazikwa katika mji alikotoka wa Al-Jouf huko nchini saudi arabia na mazishi yake yalihudhuriwa na maelfu ya watu.
Nahid alikuwa miongoni mwa maelfu ya wanafuzi wanaosoma katika chuo cha Essex amabpo inakadiriwa kuna kama wanafunzi 22365 kutoka mashariki ya kati na 9440 ni kutoka Saudi Arabia. Kuna majadiliano mengi kuhusiana na kifo cha huyu dada lakini inasemekana mwanafuzi huyu alikuwa kavaa "hijab" na "abaya" hivyo kumfanya ajulikane kuwa ni muislamu. Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini inadhaniwa huenda chuki dhidi ya uislamu ikawa ndio sababu kuu ya mauaji haya. vyombo vingi vya habari vya masharik ya kati vimeeleza kwa uwingi habari hii na wengi wao wanaamini ni kwasababu vyombo vya habari vya magharibi vimekuwa mstari wa bele kuuelezea uislamu kwa ubaya hivyo kuchangia chuki hizi dhidi ya uislamu. Cha kusikitisha ni kuwa vyombo vya habari vya magharibi havijaipa kipaumbele habari hii.
Kifo cha Nahid Almanea ni cha kusikitisha ambacho kimepeleka huzuni kubwa katika familia yake. Huenda mashambulizi haya yakaongezeka maradufu ikiwa chuki dhidi ya uislamu na waislamu vitaachwa kuendelea kusambazwa hususan kupitia vyombo vya habari. matukio haya yatachangia kwa kiasi kikubwa waswasi miongoni mwa watalii na wawekezaji kutoka mashariki ya kati na pia kwa waislamu zaidi ya milioni 3 wanaoishi ndani ya Uingereza.
Chanzo: www.middleeastmonitor.com
picha ya Nahid Almanea kwenye CCTV kabla ya kuuwawa
maelfu ya watu kwenye mazishi ya marehemu Nahid Almanea mjini kwao huko Al-jouf
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO