Sunday, April 14, 2013

RAIS WA PALESTINA AKUBALI KUJIUZUU KWA W/MKUU

Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Salam Fayyad amejiuzulu baada ya kuhudumu kwenye wadhifa huo tangu 2007. Habari zinasema kuwa, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas amekubali barua ya kujiuzulu Waziri Mkuu huyo ingawa amemtaka kubakia katika nafasi hiyo hadi pale Waziri Mkuu mpya atakapoteuliwa. Uhusiano wa Fayyad na Abbas umekuwa wa mkwaruzano katika siku za hivi karibuni. Mwezi uliopita, Fayyad alikubali barua ya kujiuzulu Waziri wa Fedha, Nabil Qassis lakini Abbas akakataa kuipokea barua hiyo. Hata hivyo hatua ya Waziri Mkuu huyo ya kujiuzulu si jambo geni kwani mara kadhaa amekuwa akiandika barua ya kujiuzulu lakini kutokana na mashinikizo ya Marekani amekuwa akilazimika kubakia ofisini. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO