Thursday, June 26, 2014

MWANAFUNZI WA CHUO KUTOKA SAUDI ARABIA AUWAWA UINGEREZA


Inna Lillahi Wainna Ilayhi Raajiuun...........Nahid Almanea alikuwa ni mwanafunzi wa shahada ya pili  kutokea Saudi Arabia  wakati akiuwawa katika mashambulizi mabaya wiki iliyopita huko Colechestor, Essex nchini Uingereza. Msichana huyu alichomwa na kitu chenje ncha kali mara 16 katika mwili wake wakati akipita katika mitaa ya jiji hilo. Polisi bado wanaendelea na msako wa waliohusika na mashambulizi hayo. Tayari dada huyu ameshazikwa katika mji alikotoka wa Al-Jouf huko nchini saudi arabia na mazishi yake yalihudhuriwa na maelfu ya watu.

Nahid alikuwa miongoni mwa maelfu ya wanafuzi wanaosoma katika chuo cha Essex amabpo inakadiriwa kuna kama wanafunzi 22365 kutoka mashariki ya kati na 9440 ni kutoka Saudi Arabia. Kuna majadiliano mengi kuhusiana na kifo cha huyu dada lakini inasemekana mwanafuzi huyu alikuwa kavaa "hijab" na "abaya" hivyo kumfanya ajulikane kuwa ni muislamu. Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini inadhaniwa huenda chuki dhidi ya uislamu ikawa ndio sababu kuu ya mauaji haya. vyombo vingi vya habari vya masharik ya kati vimeeleza kwa uwingi habari hii na wengi wao wanaamini ni kwasababu vyombo vya habari vya magharibi vimekuwa mstari wa bele kuuelezea uislamu kwa ubaya hivyo kuchangia chuki hizi dhidi  ya uislamu.  Cha kusikitisha ni kuwa vyombo vya habari vya magharibi havijaipa kipaumbele habari hii. 

Kifo cha Nahid Almanea ni cha kusikitisha ambacho kimepeleka huzuni kubwa katika familia yake. Huenda mashambulizi haya yakaongezeka maradufu ikiwa chuki dhidi ya uislamu na waislamu vitaachwa kuendelea kusambazwa hususan kupitia vyombo vya habari. matukio haya yatachangia kwa kiasi kikubwa waswasi miongoni mwa watalii na wawekezaji kutoka mashariki ya kati na pia kwa waislamu zaidi ya milioni 3 wanaoishi ndani ya Uingereza. 

Chanzo: www.middleeastmonitor.com


picha ya Nahid Almanea kwenye CCTV kabla ya kuuwawa


 
 maelfu ya watu kwenye mazishi ya marehemu Nahid Almanea mjini kwao huko Al-jouf




AL-QAEDA WASHAMBULIA UWANJA WA NDEGE WA YEMEN

Muda mfupi uliopita inasemekana wanamgambo wa Al-Qaeda wamehusika na shambulizi la uwanja wa ndege wa Yemen. Shambulizi limeathiri mnara wa kuongozea ndege, haya yamesemwa na viongozi wa ulinzi katika uwanja huo. Walinzi hao wanasema shambulizi hilo katika uwanja wa ndege wa Sayoun uliopo katika jimbo la kusini la mji wa Hadramawt lilanza kutoka maeneo matatu tofauti mapema Alhamisi ya leo.
Kutokana na shirika la utangazaji la AFP wanataarifu kuwa mpaka sasa wanajeshi watatu wameshafariki kutokana na shambulizi hilo japokwa kituo cha utangazaji cha aljazeera hawajathibitisha habari hizo. Inasemekana shambulizi hilo limetokea saa chache baada ya walinzi kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi katika mji huo unaojulikana kuwa miongoni mwa ngome kuu za wanamgambo wa Al-Qaeda.  

Chanzo: Al-Jazeera


Sunday, April 27, 2014

(SCHOLARSHIPS) NAFASI ZA KUSOMA NCHINI TURKEY!!!!

Je, unahitaji kwenda kusoma nchini Turkey? Bado hujapitwa, wahi sasa kwani wakati ndio huu. Turkey ni miongoni mwa nchi zilizoendelea duniani inayopatikana kati ya bara la Europe na Asia. Mpaka sasa kuna wanafunzi wengi sana kutoka nchi mbalimbali duniani wanaosoma nchini humo ikiwemo watanzania wengi wanaopatikana katika miji mbali mbali ya nchi hiyo kama Istanbul, Ankara, Izmir na miji mingine. Kuna vyuo vingi sana vya kisasa, hivyo serikali ya Uturuki imetoa nafasi nyingi sana (scholarships) katika vyuo vilivyopo nchini humo kwa wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma huko katika fani mbali mbali. Vipo vyuo vinavyotoa mafunzo kwa kituruki na vingine kwa kingereza. Lakini moja ya masharti yao ni lazima usome kituruki ukiwa mwanafunzi nchini humo. Lugha hii sio ngumu pindi utakapoingia darasani na kuisoma. Wapo wanafunzi wengi kutoka nchi mbali mbali wamejifunza na wanaijua vizuri lugha hii. Miongoni mwa huduma utakazopewa ni pamoja na ada ya shule, ticket ya kwenda na kurudi kutokea nchini mwako , hostel na mengine mengi. Kumbuka kabla ya kuchagua chuo, hakikisha kinatambuliwa na TCU ili usije pata matatizo pindi utakapomaliza masomo yako na kurudi Tanzania. Pia maombi yote yafanyike mtandaoni kupitia website halali iliyoidhinishwa na wizara ya nchi hiyo ambayo ni www.turkiyeburslari.gov.tr. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 19/05/2014. Unaweza  kubofya hapa kutazama video ni jinsi gani ya kutuma maombi kwa urahisi. Kutokana na kuwa ni watu wengi duniani wanaofuatilia website hiyo inaweza kuwa inasumbua kufunguka kwa kipindi fulani, hivyo endelea kuifungua kila mara mpaka pale itakapokubali. Pia unaweza kufatilia taarifa zao za kila mara kupitia ukurasa wao wa Facebook hapa. KILA LA KHERI!!!!! 

Sunday, March 16, 2014

FIRST SMV ISLAMIC SCIENTIFIC CONFERENCE AT NSSF WATER FRONT

       Deputy Minister of health Dr. Kebwe S. Kebwe at SMV first Islamic scientific conference




    Prof. Said Aboud (MUHAS), one of the presenters at SMV conference today on plenary session
            Dr. Said Kuganda from MNH presenting on anxiety disorder among HIV client
Dr. Omary Ubuguyu from MNH presenting Change in health related quality of life among Methadone Maintance Client on SMV conference today.

            Dr. Zubeda SMV organizing Chair person presenting her part on Conference today.

 Dr.Ali Mzige left,Dr. Bushiri Tamim at righgt (former TIMA leaders) and Dr. Juma Mwimbe (SMV secretary) on the way foreward session.






                                            Other participants at the Conference of SMV

Wednesday, March 05, 2014

Entering Jannah because of Your Deeds or ALLAH'S mercy



The prophet - peace and blessing upon him - said:

“No one will enter jannah (heaven) for his deeds ('بعمله')!”

People said: “even you, messenger of Allah?”

“Even me!” he said, “unless Allah wraps me with His mercy”.

So, how to concord between this hadeeth and the other texts indicating that a person will enter Jannah for his actions?

The scholars - may Allah have mercy on them - who are the most descerning of the rules of islam, and who are the doctors of the hearts and the bodies, taught by Allah, said:

" the 'for' (the 'ب' in 'بعمله') appeared in "for his deeds" can have two meanings:

it can be used for causality (because of), and it can also be used for substitution (in return for / as equivalent for). "

So, if you say: “I sold you this book for one dirham”, this is for substitution.

And if you say: “I honor you, for you have honored me”. This one is for causality.

As for the fact of entering Jannah for our deeds, it is rather about causality and not substitution.

They (the scholars) said: " the meaning of the hadeeth of the prophet - peace and blessing be upon him - : "no one will enter Jannah for his deeds" is meant to deny the substitution.

Because, if Allah - Almighty - wanted to give people a reward exactly equivalent to their good actions, then one single grace of Allah in this life should have overweighed all their good deeds. "

I give the example of the gift of breathing:

It's a great gift, and no one is really aware how great it is, except the people who suffer from breathing difficulties, and you can ask those people having this disease how much pain they experience from it.

And the hale person who is not affected by this disease does not feel the slightest inconvenience while he is enjoying this gift, so he can breathe while talking and when he is eating and he does not feel anything.

That gift, no matter how many good deeds you made, you will not recompense it, for it's a continuous and permanent gift.

And (also) we say, if you are guided to do good deeds, then this (guidance) – itself - is a grace given to you by Allah, from which too many people are strayed.

And if every grace requires a thanking, then your ability to thank Allah for a grace He gave you is it a grace which needs another thanking, and so on.

Monday, September 30, 2013

THE QURAN HAS ALL THE ANSWERS


Why am I always being tested? Why is life so hard? Why don't I ever get this or that? Why? Why?
I am always asking: Why was I tested?
Quran answers: “Do men think that they will be left alone saying, ’We believe’, and that they will not be tested? We did test those before them, and Allah will certainly know those who are true from those who are false.” [29:2-3]
I am always asking: Why could I never get what I want?
Quran answers: ”It is possible that you dislike a thing which is good for you, and that you love a thing, which is bad for you. But Allah knows, while you know not.” Surah Al-Baqarah [2:216]
I am always asking:Why was I burdened this way?
Quran answers: “Allah does not place a burden to a soul greater than it can bear. It gets every good that it earns, and it suffers every ill that it earns.” Surah Al-Baqarah [2:286] & “So verily, with every difficulty there is relief: (repeated) Verily, with every difficulty there is relief.” Surah Al-Insyirah [94:5-6]
I am always asking: Why do I lose hope?
Quran answers: “So lose not heart, nor fall into despair…” Surah Al-Imran [3:139]
i am always asking: How can I face it?
Quran answers: ” O you who believe! Persevere in patience and constancy; vie in such perseverance; strengthen each other; and fear Allah that you may prosper.” Surah Al-Imran [3:200] & “And seek (Allah’s) help with patience, perseverance and prayer: It is indeed hard, except to those who bring a humbly submissive (to Allah).” Surah Al-Baqarah [2:45]
i am always asking: What do I get for all these?
Quran answers: “Indeed, Allah has purchased from the believers their lives and properties (in exchange) for that they will have the garden (of Paradise)…” Surah At-Taubah [9:111]
I am always asking:To whom can I depend?
Quran answers: “(Allah) suffices me: there is no god but He: On Him is my trust- He the Lord of the Throne (of Glory) Supreme.” Surah At-Taaubah [9:129]
i always say:But I can’t take it anymore!
Quran answers: “…and never give up hope of Allah’s Soothing Mercy; truly No one despairs of Allah’s Soothing Mercy. except Those who have no faith.” Surah Yusuf [9:87] & “Despairs not of the Mercy of Allah: for Allah forgives All sins for He is Often- For giving, Most Merciful.” Surah Az-Zumar [39:53].


Article by brother

                 Mgaya S Mgaya

Sunday, August 25, 2013

PENTAGON YASEMA IKO TAYARI KWA LOLOTE JUU YA SYRIA

Chuck Hagel Waziri wa Ulinzi wa Marekani amekariri kwamba Pentagon imejitayarisha kuchukua chaguo lolote la dharura dhidi ya Syria na ipo tayari kutumia nguvu iwapo Rais Barack Obama ataidhinisha suala hilo.Hagel amesema kwamba, Rais Obama ameitaka Wizara ya Ulinzi ya Marekani kujitayarisha kwa chaguo lolote lile litakalowezekana kuchukuliwa dhidi ya Syria.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani ameongeza kuwa, maafisa wa Marekani wanachunguza suala la kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Rais Bashar al Assad kutokana na ripoti ya kufanyika mashambulizi ya silaha za kemikali katika vitongoji vya Damascus wiki iliyopita.Hata hivyo ripoti zinasema kwamba, mashambulizi hayo ya silaha za kemikali yamefanywa na waasi wa Syria wanaoungwa mkono na nchi za Ulaya,  Marekani  na baadhi ya nchi za Kiarabu.

RAIS WA YEMEN AUNGA MKONO DRONE KUTUMIKA NCHINI HUMO

Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi wa Yemen ameunga mkono mashambulizi ya mauaji ya ndege za Marekani zisizo na rubani yaani "drone" nchini humo. Mansur Hadi ameeleza kuwa mashambulizi ya drone za Marekani yanatekelezwa  kulingana na makubaliano yaliyosainiwa kati ya Washington na Ali Abdullah Saleh dikteta wa zamani wa Yemen baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001.
Rais wa Yemen amesema hatua ya nchi yake ya kushirikiana na Marekani katika mapambano ya kile alichokitaja kuwa  dhidi ya ugaidi siyo siri. Ameongeza kuwa Yemen ina maafisa wake wa kijeshi katika vituo vya kuendeshea mashambulizi hayo ya drone nchini Djibouti na Bahrain. Marekani imekuwa ikikosolewa vikali kutokana na hatua yake ya kuzidisha mashambulizi ya ndege zisizo na rubani huko Yemen, ambako raia wa nchi hiyo wamekuwa wakiandamana mara kwa mara wakilaani hatua ya Washington ya kukiuka mamlaka ya kujitawala ya Yemen.

MAREKANI YALAANI SHAMBULIZI LA LEBANON

Serikali ya Marekani imelaani shambulizi lililotokea huko Lebanon na kusababisha vifo vya watu 42 mpaka sasa huku mamia wakijeruhiwa baada ya magari yalokuwa yameegeshwa nje ya msikiti kulipuliwa mjini Tripoli. Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani Susan Rice ameandika kupitia mtandao wa Twita kuwa Marekani imelaani vikali shambulizi hilo na kutoa pole kwa majeruhi na ndugu za watu wasiokuwa na hatia ambao walipoteza maisha yao. Mashambulizi hayo mawili yamejiri wakati wa ibada za waislamu mjini Tripoli ambapo wafuasi wa Suni ambao wanaunga mkono waasi wa Syria wamekuwa wakihusishwa na ghasia za mara kwa mara dhidi ya wale wanaomuunga mkono raisi wa Syria Bashar al Assad.
Serikali ya Washington mara kadhaa imevunja ukimya juu ya machafuko ya Syria na kuenea katika maeneo kadhaa na hususan kuvuruga amani ya lebanon. Naibu Msemaji wa serikali Marie Harf ametoa wito kwa pande zote mbili nchini Lebanon kuwa watulivu.

KIONGOZI WA WAASI SUDAN ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS

Raisi wa Sudani Kusini Salva kiir amemteua kiongozi wa zamani wa waasi James Wani Iga kuwa makamu wake,vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimearifu. Igga, ambaye amekuwa spika wa bunge la Sudan kusini tangu 2005 ameonekana kuwa chaguo linalosawazisha tofauti ya kikabila kati ya viongozi wa taifa na itasaidia sana hali ya mambo kuelekea uchaguzi mwaka 2015.
Igga ambaye ni Naibu mwenyekiti wa chama cha SPLM anatokea katika kabila la Bari ambao ni wenyeji wa eneo la Juba. Mwezi uliopita raisi Kiir alichukua hatua ya kushangaza baada ya kuvunja Baraza la Mawaziri na kisha kumfuta kazi Makamu wa Rais Riek Machar kitu kilichotajwa kuchangiwa na tofauti za kisiasa baina yao. Makamu mpya wa Rais Kiir anatarajiwa kushauriana naye kuunda Baraza jipya la Mawaziri.

RAFAH YAFUNGULIWA TENA

Serikali ya mpito ya Misri leo imekifungua tena kivuko cha Rafah kilichoko kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na eneo la Ukanda wa Gaza la ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Maelfu ya Wapalestina wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu na wagonjwa wanaohitaji kupatiwa matibabu nje ya Ukanda wa Gaza walikuwa wameshindwa kuelekea huko Misri huku mamia ya Wapalestina waliokuweko nchini humo wakishindwa kurejea makwao kutokana na kufungwa njia hiyo pekee ya mpakani kwa wakaazi wa Gaza. Uhusiano kati ya serikali halali ya Palestina inayoongozwa na HAMAS yenye makao yake Ukanda wa Gaza na serikali ya mpito ya Misri umekuwa wa kusuasua tangu jeshi lilipomuondoa madarakani rais Muhammad Morsi aliyekuwa muitifaki mkubwa wa HAMAS. Maher Abu Sabha, afisa anayesimamia kivuko cha Rafah kwa upande wa Palestina amesema mamlaka za Misri zinakifungua kivuko hicho kwa muda wa saa chache tu kwa siku. Maafisa wa HAMAS wameilalamikia hatua ya serikali ya Misri ya kupunguza kiwango cha watu wanaoruhusiwa kupita kwenye kivuko cha Rafah kutoka watu 1,200 hadi 300 kwa siku tangu Julai 3 wakati jeshi lilipomuondoa madarakani Morsi. Tangu mwaka 2007, utawala wa Kizayuni umeshadidisha mzingiro dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza na kusababisha maafa na matatizo makubwa kwa wananchi hao.

WAISLAM NIGERIA WAANDAMANA KUTAKA MORSI KUREJESHWA

Maelfu ya Waislamu wameandamana kwa amani kaskazini mwa Nigeria leo kutaka kurejeshwa madarakani kwa Rais wa Misri Mohammed Mursi aliyepinduliwa na jeshi mwezi uliopita.Kiasi ya waandamanaji 4,000 waliokuwa wamebeba mabango waliimba nyimbo za kumsifu Mursi nje ya msikiti katika mji wa Kano.Waandalizi wa maandamano hayo wanasema takriban waandamanaji 5,000 walishiriki.Kiongozi wa maandamano hayo sheikh Abubakar Mujahid amewaambia wanahabari kuwa wanataka kuachiliwa huru kwa Mursi na wafungwa wengine wa kisiasa wanaozuiliwa na serikali ya muda ya Misri.Nigeria taifa lililo na idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika ya kiasi ya watu milioni 160 limegawanyika nusu kwa nusu ambapo Waislamu wanaishi hasa kaskazini  na Wakristo wanaokaa zaidi kusini mwa nchi hiyo.

Saturday, August 24, 2013

WANANCHI WA CONGO WAANDAMANA

Mamia ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameandamana kupinga mashambulizi yanayowalenga wakati wa makabiliano kati ya wanajeshi wa kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa na wapiganaji wa kundi la waasi la M23 katika mji wa Goma ulioko mashariki mwa nchi hiyo.Mwanamke mmoja na watoto wawili waliuawa mapema leo asubuhi katika mji huo wa Goma ambao ndio mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini.Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakijibu mashambulizi ya waasi wa M23 tangu Jumatano.Msemaji wa kikosi hicho maalumu Luteni Colonel Felix Prosper Basse amesema hali katika eneo hilo ni tete mno na kwamba shambulio hilo la hivi karibuni kabisa halikubaliki kamwe kwani linawalenga raia. Mapigano hayo yamewalazimu kiasi ya watu laki nane kutoroka makwao.Umoja wa Mataifa umetuma kikosi maalum cha wanajeshi 3,000 mashariki mwa Congo hususan kukabiliana na makundi ya waasi.Basse amesema wanashirikiana na wanajeshi wa nchi hiyo kuhakikisha usalama wa raia unadumishwa na kuahidi shambulio kama hilo halitafanyika tena.