Assalam alaykum warahmatul lahi wabarakatuh.
Ndugu zangu napenda kuwataarifu kuwa muda wa kujaza form/ kuapply katika mavyuo kwa ndugu zetu wa form six na form four umefika na baadhi ya mavyuo wameshatoa form watu wajaze.
Cha muhimu ni kuwahi kufuatilia hizo form na kujaza kabisa mapema ili tusijeanza kukimbizana baadae. Pia kwa form six jambo lingine ni kuwa TCU karibu wanaanza kufungua ukumbi watu wapply hilo nalo tulifuatilie mapema nalo ili kama kuna kasoro turekebishe kabla ya ya siku ya mwisho ya kuapply.
Pia kwa ndugu yeyote anayesoma hii nakala basi ni vizuri pia awafikishie waislam wengine hususani waliomaliza form six.
Katika hii blog kuna post ya November mwaka jana inawebsite ya TCU kwa ajili ya watu kuitumia na kuangalia mavyuo ambayo yapo chini ya TCU, pi kuna wizara ya afya watu wadownload form na kujaza na kuzifikisha panapo husika. Kwa maswali zaidi kwa wale wa Dar es salaam ni bora wafike makao makuu yetu ambayo ni MUHIMBILI CHUO CHA AFYA wafike msikitini na kuulizia AMIR AU KATIBU wa jumuiya ya wanafunzi wa kiislam na hapo atatupata wahusika tukiwa na detail ambazo zinaweza kukufaa wewe au ukafikisha kwa wengine na wale wa mikoani bado hatujawa na wajumbe rasmi ila unaweza kuwasiliana nasi kwa njia ya simu(kuna nakala imeandikwa form six na form four ya NOvember pia chini kabisa kuna majina na namba za simu, facebook tafuta MSAMU MUHIMBILI tuma ujumbe wako, au katika hii blog tuma kwa njia ya comment na tutajaribu kushughulikia kadri ALLAH atavyotuwezesha. Pia kuna chuo kipo njia ya tegeta AL- MAKTOUM COLLEGE OF ENGINEERING AND TECHNOLOGY nao pia wanatoa form za kujiunga.
Shime waislam tukumbushane sisi kwa sisi kwani makafiri wenzetu wanamavyuo yao hata wakikosa vya serikali wanakwenda kusoma vyuo vyao lakini sisi bado tuko nyuma hivyo insha allah tujitahidi kukumbusha kufuatilia haya masuala kwani faida ipo ingawa unaweza usiione kwa macho ya karibu.
INSHA ALLAH ALLAH ATUFANIKISHIE HILI NA MENGINEYO MAASSALAM.
Tuesday, February 28, 2012
Friday, February 10, 2012
NINI TUNAJIFUNZA KAMA WAISLAM TUNAOTAKA MABADILIKO.
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) iliyofanyika nchini Oktoba, mwaka jana, huku kiwango cha kufaulu kikionyesha kuwa kiasi cha asilimia 46.63 na cha kufeli kwa kupata daraja sifuri ni asilimia 53.37
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Joyce Ndalichako, yanaonyesha kuwa, licha ya kiwango cha kufaulu kuongezeka kwa asilimia 3.13, bado wanafunzi wengi wameendelea kufanya bibaya katika mtihani huo.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, kati ya watahiniwa 426,314 sawa na asilimia 94.67 waliofaulu kati ya daraja la kwanza hadi la nne ni 180,216.
Hata hivyo, waliofaulu kwa daraja la nne ndio wengi wakiwa ni 146,639 sawa na asilimia 81.3 ya waliofaulu huku wale wa daraja la kwanza, pili na tatu wakiwa ni 33,577 sawa na asilimia 9.8.
Wakati hali kwa watahiniwa ikiwa hivyo, shule za sekondari za kata, zimeendelea kufanya vibaya kulinganisha na zile za watu binafsi.
Pia watahiniwa 3,303 wamefutiwa matokeo kutokana na baadhi kufanya udanganyifu na wengine kuandika matusi katika karatasi zao za majibu ya mitihani.
Hata hivyo, matokeo hayo yanaonyesha wavulana wakiongoza kufaulu mitihani hiyo kwa asilimia 53.53, huku wasichana wakifaulu kwa asilimia 44.36.
WATAHINIWA WA SHULE WALIOFAULU MTIHANI
“Mwaka 2010 watahiniwa waliofaulu walikuwa 177,021 sawa na asilimia 50.40 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo. Hivyo, kiwango cha kufaulu kimeongezeka kwa asilimia 3.13,” alisema Dk. Ndalichako. Ongezoko hilo ni sawa na watahiniwa 12,789.
WATAHINIWA WOTE
Alisema jumla ya watahiniwa 225,126 (asilimia 53.37) wamefaulu mtihani huo, wakiwamo wasichana 90,885 sawa na asilimia 48.25 ya wasichana waliofanya mtihani na wavulana 134,241 sawa na asilimia 57.51 ya wavulana waliofanya mtihani.
“Mwaka 2010 watahiniwa waliofaulu walikuwa 223,085 sawa na asilimia 50.74. hivyo, kufaulu kumeongezeka kwa asilimia 3.13,” alisema Dk. Ndalichako.
WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI
Alisema jumla ya watahiniwa 450,324 walisajiliwa kufanya mitihani hiyo, kati yao wakiwamo wasichana 201,799 (aslimia 44.81) na wavulana 248,525 (asilimia 55.19), idadi ambayo imepungua kwa watahiniwa 7,790 (asilimia 1.70) kati ya watahiniwa 458,114 waliosajiliwa mwaka juzi.
WALIOFANYA NA AMBAO HAWAKUFANYA MTIHANI
Dk. Ndalichako alisema watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 426,314 (asilimia 94.67) na kwamba, watahiniwa 24,010 hawakufanya mtihani, ambao ni sawa na asilimia 5.33 ya watahiniwa wote waliosajiliwa.
WATAHINIWA WA SHULE WALIOSAJILIWA
Alisema watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 349,390 wakiwamo wasichana 150,371 (asilimia 43.04) na wavulana 199,019 (asilimia (56.96), idadi ambayo inaonyesha kupungua kwa watahiniwa 14,209 (asilimia 3.91) kati ya watahiniwa 363,589 wa shule waliosajiliwa mwaka juzi.
VITUO VYA MITIHANI
Dk. Ndalichako alisema jumla ya vituo 4,795 vilitumika katika kufanya mitihani hiyo ikilinganishwa na vituo 4,653 vilivyotumika mwaka juzi.
WALIOFAULU MTIHANI WA MAARIFA
Alisema katika Mtihani wa Maarifa (QT) wa mwaka jana, jumla ya watahiniwa 9,069 (asilimia 40.70) ya waliofanya mtihani wamefaulu ikilinganishwa na asilimia 35.17 ya waliofaulu mtihani mwaka juzi.
“Hivyo, kiwango cha kufaulu kwa Mtihani wa Maarufu kimeongezeka kwa asilimia 5.53 ikilinganishwa na mwaka 2010,” alisema Dk. Ndalichako.
Alisema katika mtihani huo, watahiniwa waliosajiliwa ni 29,447 ambapo wasichana walikuwa ni 18,019 na wavulana ni 11,428 na kwamba, jumla ya watahiniwa 22,400 (asilimia 76.07) ya waliosajiliwa wamefanya mtihani, wasichana wakiwa ni 13,898 na wavulana ni 8,502.
WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA
Dk. Ndalichako alisema watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 44,910 (asilimia 52.52) ya waliofanya mtihani; wasichana wakiwa ni 20,972 (asilimia 47.90) na wavulana ni 23.938 (asilimia 57.38).
Alisema mwaka juzi watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 46,064 (asilimia 52.09) walifaulu mtihani huo.
UBORA WA KUFAULU KWA JINSIA
Dk. Ndalichako alisema jumla ya watahiniwa wa shule 33,577 (asilimia 9.98) wamefaulu katika madaraja I-III; wasichana wakiwa 10,313 (asilimia 7.13 na wavulana 23,264 (asilimia 12.13).
SHULE BORA
Alizitaja shule 10 bora zilizoko katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni St. Francis Girls iliyoko mkoani Mbeya; Feza Boys (Dar es Salaam); St. Joseph Millenium (Dar es Salaam); Marian Girls (Pwani); Don Bosco Seminary (Iringa); Kasita Seminary (Morogoro); St. Mary’s Mazinde Juu (Tanga); Canossa (Dar es Salaam); Mzumbe (Morogoro) na Kibaha (Pwani).
Pia alizitaja shule 10 bora zilizoko katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 40 kuwa ni Thomas More Machrina (Dar es Salaam); Feza Girls (Dar es Salaam); Dung’unyi Seminary (Singida); Maua Seminary (Kilimanjaro); Rubya Seminary (Kagera); St. Joseph Kilocha Seminary (Iringa); Sengerema Seminary (Mwanza); Lumumba (Unguja); Queen of Apostels-Ushirombo (Shinyanga) na Bihawana Junior Seminary (Dodoma).
SHULE ZA MWISHO
Vilevile, alizitaja shule 10 za mwisho zenye watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni Bwembwera (Tanga); Pande Darajani (Tanga); Mfundia (Tanga); Zirai (Tanga); Kasokola (Rukwa); Tongoni (Tanga); Mofu (Morogoro); Mziha (Morogoro); Maneromango (Pwani) na Kibuta (Pwani).
Kadhalika, alizitaja shule 10 za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40 kuwa ni Ndongosi (Ruvuma); St. Luke (Ruvuma); Igigwa (Tabora); Kining’inila (Tabora); Ndaoya (Tanga); Kilangali (Morogoro); Kikulyungu (Lindi); Usunga (Tabora); Mto Bubu Day (Dodoma) na Miguruwe (Lindi).
WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI ZAIDI
Aliwataja watahiniwa 10 bora kitaifa kuwa na shule wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Moses Andrew Swai (Feza Boy’s-Dar es Salaam); Rosalyn Tandau (Marian Girls-Pwani); Mboni Maumba (St. Francis Girls-Mbeya); Sepiso Mwamelo (St. Francis Girls-Mbeya); Uwella Rubuga (Marian Girls-Pwani); Hellen Mpanduji (St. Mary’s Mazinde Juu-Tanga); Daniel Wallace Maugo (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Benjamin Tilubuzya (Thomas More Machrina-Dar es Salaam); Simon William Mbangalukela (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam) na Nimrod Deocles Rutatora (Feza Boy’s-Dar es Salaam).
WASICHANA 10 BORA KITAIFA
Pia aliwataja wasichana 10 bora kitaifa kuwa ni Rosalyn Tandau (Marian Girls-Pwani); Mboni Maumba (St. Francis Girls-Mbeya); Sepiso Mwamelo (St. Francis Girls-Mbeya); Uwella Rubuga (Marian Girls-Pwani); Hellen Mpanduji (St. Mary’s Mazinde Juu-Tanga); Lissa Chile (St. Francis Girls-Mbeya); Elizabeth Ng’imba (St. Francis Girls-Mbeya); Doris Atieno Noah (Kandoto Sayansi Girls-Kilimanjaro); Herieth Machunda (St. Francis Girls-Mbeya) na Daisy Mugenyi (Kifungilo Girls-Tanga).
WAVULANA 10 BORA KITAIFA
Vilevile, aliwataja wavulana 10 bora kitaifa kuwa ni Moses Andrew Swai (Feza Boy’s-Dar es Salaam); Daniel Wallace Maugo (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Benjamin Tilubuzya (Thomas More Machrina-Dar es Salaam); Simon William Mbangalukela (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Nimrod Deocles Rutatora (Feza Boy’s-Dar es Salaam); Simon Gabriel Mnyele (Feza Boys-Dar es Salaam); Paschal John Madukwa (Nyegezi Seminary-Mwanza); Henry Justo Stanley (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Frasisco Paschal Kibasa (Mzumbe-Morogoro) na Tumaini Charles (Ilboru-Arusha).
MATOKEO YA MTIHANI YALIYOSITISHWA
Katibu Mtendaji huyo alisema Baraza limesitisha kutoa matokeo ya watahiniwa 264 wa kujitegemea waliofanya mtihani wa kidato cha nne, 116 waliofanya mtihani wa maarifa na 873 wa shule za binafsi mwaka jana bila kulipa ada ya mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini.
Alisema ikiwa watahiniwa hao hawatalipa baada ya miaka miwili tangu matokeo yatakapotangazwa, matokeo yatafutwa.
Dk. Ndalichako alisema wengine ni watahiniwa 67 ambao hawajawasilishiwa alama za tathmini ya masomo (Continuous Assessment) katika masomo yote waliyofanya hadi hapo Mkuu wa Shule husika atakapowasilisha pamoja na sababu za kutowasilisha mapema.
WALIOFANYA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI
Alisema Baraza pia limefuta matokeo ya watahiniwa 3,303 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba mwaka jana; ambao kati yao alisema watahiniwa 3,301 ni wa mtihani wa kidato cha nne na wawili ni wa maarifa.
Alizitaja aina za udanganyifu zilizobainika kufanywa na watahiniwa hao kuwa ni pamoja na watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na notes, simu kufanyiwa mitihani na watu wengine na kubainika wamesajiliwa kufanya mtihani kwa kutumia majina ya wengine wakati walishafanya mtihani.
Aina nyingine za udanganyifu ni watahiniwa kubainika kuwa na mfanano wa majibu usio wa kawaida, kuwa na karatasi zao kuwa na miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika katarasi ya somo moja, kubadilishana karatasi za maswali/vijitabu vya kujibia mtihani ili kuandikiana majibu, au kujadiliana ndani ya chumba cha mtihani.
Pia watahiniwa kukamatwa na vijitabu vya kuandika mitihani zaidi ya moja ambayo moja hakupewa na msimamizi, kubainika kuwa na kesi mbili tofauti; kama vile, mfanano wa majibu, notes, kijitabu cha kujibia zaidi ya kimoja na kubadilishana karatasi ya majibu au kijitabu cha kujibia mtihani.
WATAHINIWA WALIOANDIKA MATUSI
Dk. Ndalichako alisema matokeo mengine yaliyofutwa na Baraza ni ya watahiniwa wanane walioandika matusi katika karatasi za majibu yao.
Alisema kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5 (13) cha kanuni za mtihani.
Dk. Ndalichako alisema kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu, kinaonyesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu na kwamba Baraza halitavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo.
“Hivyo, pamoja na kuwafutia matokeo ufuatiliaji zaidi utafanyika ili kuona hatua zaidi wanazoweza kuchukuliwa,” alisema Dk. Ndalichako.
Aliwataka watahiniwa walioanza mitihani ya kidato cha sita jana kujiepusha na udanganyifu katika mitihani na pia kuepuka mtindo wa kuandika matusi katika skripti zao au mambo yasiyohusiana na mtihani.
HATMA YA WATAHINIWA WALIOFUTIWA MATOKEO
Alisema Baraza limekuwa likifuta matokeo ya watahiniwa wanaofanya udanganyifu, lakini idadi ya wanaojihusisha na vitendo hivyo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
“Hivyo, katika kikao chake cha 86 kilichofanyika tarehe 7/2/2012, Baraza liliamua kuwa watahiniwa wote waliofutiwa matokeo yao kutokana na kujihusisha na udanganyifu au kuandika matusi kwenye karatasi zao za majibu hawataruhusiwa kufanya mtihani wa Baraza kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu,” alisema Dk. Ndalichako.
VITUO NA WALIOHUSIKA NA UDANGANYIFU
Alitoa onyo kali kwa wamiliki wote wa vituo na shule ambazo zimejihusisha na udanganyifu.
“Tunapenda kuwajulisha wamiliki wote wa vituo vya watahiniwa wa kujitegemea kuwa ni wajibu ao kuhakikisha kuwa kanuni zote za uendeshaji mitihani zinazingatiwa ipasavyo,” alisema Dk. Ndalichako.
CHANZO: NIPASHE
Wednesday, February 08, 2012
VALENTINE DAY
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu was Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa ‘Aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa Ba’ad,
Allaah سبحانه وتعالى Ametuchagulia dini ya Kiislamu ambayo ndio dini ya haki na Hatokubali dini yoyote nyingine kama Anavyosema:
((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))
((Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasirika)) [Al-'Imraan:85]
Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالى katika desturi na mila zao kama ifuatavyo:
((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم
((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) Al-Bukhariy na Muslim
Maneno hayo aliyoyasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakika yamesadikika kwani tunaona jinsi gani Waislamu siku hizi wanavyoigiza mila, desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii inayoitwa 'Valentine day' (Siku ya Wapendanao).
Na baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe (e-mail), salamu katika simu za mkono. Hakika fitna hii humfanya Muislamu aharibu 'Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika sheria ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.
-Historia Ya Sherehe Ya Siku Ya Valentine
Hii ni sherehe ya wapagani wa Kirumi wakati dini yao ya upagani ilikuwa ni dini iliyotapakaa kwa Warumi karne zaidi ya kumi na saba zilizopita. Na fikra zao ilikuwa ni kuelezea hisia ya 'mapenzi ya kiroho'
Kulikuwa na visasili (uongo) zilizohusishwa na sherehe hii ya upagani ya Warumi ambao umeendelea kutoka warithi wa Kikiristo. Miongoni mwa uongo huo ni kuamini kwao Warumi kuwa Romulus, aliyevumbua Rome, alinyonyeshwa siku moja na mbwa mwitu mwanamke, hivyo akampa nguvu na hikma.
Warumi walikuwa wakisherehekea tukio hili katikati ya Februari kila mwaka kwa kufanya sherehe kubwa. Na mojawapo ya tambiko katika sherehe hii ni kuchinja mbwa au mbuzi. Vijana wawili wenye nguvu hujipaka damu ya mbwa au ya mbuzi katika miili yao, kisha huiosha damu hiyo kwa maziwa. Baada ya hapo, watu hufanya gwaride wakiwa vijana hawa wawilii wako mbele wakiongoza gwaride iliyokuwa ikitembea barabarani. Vijana hao wawili walikuwa wakichukua vipande vya ngozi ambavyo waliwapigia watu wanaowavuka. Wanawake wa kirumi walikuwa wakipokea mapigo hayo wakiamini kuwa yatawahifadhi na kutibu utasa.
Kuungamana Baina Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) Na Sherehe Hii
Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) ni jina waliopewa mashujaa wawili wakongwe waliokufa ambao ni wana wa kanisa la kikiristo. Inasemekena kwamba walikuwa ni wawili au mmoja tu. Huyo mmoja alikufa Rome kutokana na mateso ya kiongozi wa Kigothi aliyeitwa Claudius. Kanisa la Saint Valentine lilijengwa kwa ajili ya kudumisha kumbukumbu yake.
Warumi walipoingia ukristo, wakaendelea kusherehekea sikukuu ya wapendanao (valentine day) lakini wakabadilisha kutoka fikra ya upagani ya 'mapenzi ya kiroho' (spiritual love) na kuleta fikra nyingine iliyojulikana kama ni 'mapenzi ya mashujaa' yaliyowakilishwa na Saint Valentine ambaye aliuliwa kwa ajili ya kutetea mapenzi na amani. Vile vile ikajulikana ni sikukuu ya wapenzi, na Saint Valentine alifanywa kuwa ni mlezi wa mapenzi ya mtakatifu.
Miongoni mwa imani yao inayoambatana na sherehe hii ni kwamba majina ya wasichana waliofika umri wa kuolewa yaliandikwa katika vikaratasi vidogo vilivyokunjwa mviringo kisha vikawekwa katika chombo juu ya meza. Kisha wavulana waliotaka kuoa waliitwa na kila mmoja huchagua karatasi moja ikiwa na jina la msichana. Kisha hujiambatanisha naye huyo msichana aliyempata kutokana na kura hiyo aliyochagua kwa muda wa mwaka ili wajuane vizuri kisha tena hufunga ndoa, au kama hawakuelewana hurudia tena kufanya kura inapofika siku hiyo mwaka unaofatia.
Vile vile imesemekana kwamba chanzo cha sikukuu hii, ni kwamba warumi walipokuwa wakristo baada ya ukristo kutapakaa, Mfalme wa Kirumi Claudius II alitoa hukumu katika karne ya tatu kwamba askari wasioe kwa sababu kuoa kwao kutawashughulisha na vita walivyokuwa wakipigana. Hukumu hiyo ilipingwa na Saint Valentine ambaye alianzisha kuozesha maaskari kwa siri. Alipokuja kujua mfalme, alimfunga jela na akamhukumu kuuliwa. Huko jela akapendana na mtoto wa mkuu wa jela, lakini ikawa ni siri kwani kutokana na sheria ya ukristo, mapadri na makasisi wameharamishwa kuoa au kupenda.
Hata hivyo alipewa heshima yake na wakristo kwa sababu ya kushikilia na kujikita imara katika ukristo wakati mfalme alipotaka kumsamehe kwa sharti aache ukristo na kuabudu miungu ya Kirumi ili awe msiri wake na awe mkwe wake. Lakini Saint Valentine alikataa ahadi hiyo na akapendelea ukristo, kwa hiyo akauliwa siku ya tarehe 14 Februari 270 CE. Ndio ikaitwa siku hii kwa jina la huyo mtakatifu (Valentine).
Papa (Pope) naye akaifanya siku hiyo ya kufa Saint Valentine tarehe 14 Februari 270 CE kuwa ni sikukuu ya mapenzi. Na ni nani alikuwa Papa huyo? Ni Askofu mkuu wa kanisa la 'universal church', ambaye ni mrithi wa mtakatifu Peter.
Ndugu Waislamu tazameni vipi huyo askofu anavyohusika katika kuadhimisha sikukuu hii ambayo ni uzushi katika dini yao ya Kikiristo. Hii itukumbushe kauli ya Allaah سبحانه وتعالى
((اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللّهِ))
((Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu)) [At-Tawbah: 31]
Matendo Yanayotakiwa Kujiepusha Nayo Ambayo Yanayofanyika Katika Sikukuu Hii
1. Kuonyeshana bashasha na furaha kama ilivyo katika sikukuu zao nyingine.
2. Kupeana mawaridi mekundu (Red Roses) ambayo ni alama ya kuelezea mapenzi, 'mapenzi ya kiroho' ya wapagani au 'mapenzi' ya Wakristo. Hivyo inajulikana kuwa ni 'Sikukuu Ya Wapendanao'.
3. Kupelekeana kadi. Na kadi nyingine zina picha za 'mungu wa mapenzi wa kirumi' ambaye ana mbawa mbili, akiwa amekamata upinde na mshale. Huyu ndio mungu wa mapenzi wa wapagani warumi. Shirk iliyoje hii ndugu Waislamu?
4. Kubadilishana maneno ya mapenzi na matamanio katika kadi wanazopelekeana, yakiwa katika mfumo wa kimashairi, tenzi na sentensi fupi fupi. Kadi nyingine zina picha za kimzaha na maneno ya kuchekesha, na mara nyingi zina maneno ya kusema 'Kuwa Valentine wangu'. Hii inaashiria maana ya kikiristo ya sikukuu hii baada ya kuwa asili yake ni kutokana na fikra za upagani.
5. Katika nchi nyingi za kimagharibi, hufanyika sherehe siku hiyo ambayo kunakuweko kuchanganyika wanaume na wanawake, kuimba, na kucheza dansi. Na wengi wanapelekeana zawadi kama mawaridi, maboksi ya chokoleti kwa wake zao, marafiki na wanaowapenda.
Kutokana na maelezo yote hayo ya chanzo cha sikukuu hii, tunaona kwamba siku hiyo haina uhusiano wowote katika Uislamu, bali yana uhusiano na washirikina mapagani, hata wakristo katika dini yao nao pia ni uzushi, sasa itakuwaje sisi Waislamu tuwaigize kusherehekea?
Basi ndugu Waislamu tutambue kuwa jambo hili ni ovu mno, haimpasi Muislamu kuharibu 'Aqiydah (iymaan) yake kwani kuna hatari kubwa kushiriki katika sherehe hii nayo ni kuingia katika kumshirikisha Allaah سبحانه وتعالى, na kama tunavyojua kuwa Allaah سبحانه وتعالى Hamsamehe mtu anayefanya shirki pindi akifariki bila ya kutubu kama ilivyo katika aya ifuatayo:
((إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء وَمَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدِ افْتَرَى إِثْمًا عَظِيمًا))
((Hakika Mwenyezi Mungu Hasamehe kushirikishwa, na Husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa)) [An-Nisaa: 48]
Hivyo ni kuharamishwa na Pepo na kupata makazi ya moto, tunajikinga na Allaah kwa hayo.
((إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللّهُ عَلَيهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَار))
((Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru)) [Al-Maaidah: 72]
Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atuepushe na kila aina ya shirk na Atuonyeshe yaliyo ya haki tuyafuate, na yaliyo ya batili tujiepushe nayo na Atuajaalie ni miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn

Monday, February 06, 2012
Sunday, February 05, 2012
Thursday, February 02, 2012
NAAGA NDUGU NAAGA
Ya Allah Karimu, Mmiliki wa Uhai,
Nimeshika kalamu, Nafurahi nipo hai,
Leo imeniladhimu, Niage ningali hai,
Forodhani:Unguja,Buriani ikhwani.
Siku yangu ikifika, Kauli itakapo funga,
Siku yangu ikifika, Kauli itakapo funga,
Kifo kweli natamka, Jamani hakina kinga,
Oman: Uamarika, Buriani ikhwani.
Siku imefichikana, Anayejua manani,
Usiku au Mchana, Sitambui abadani,
Nafsii ya kuagana, Ameridhia manani,
Pemba Yemen Londona, buriani ikhwani.
Kama nikifa porini, Niwe mlo wa wanyama,
Au kule baharini,Samaki wanile nyama,
Mema ya mtu thamani, Roho yaishi salama,
Canada,Bahraini,Buriani ikhiwani.
Kikinifika nyumbani,Niosheni ndugu yenu,
Na sanda nivisheni, Nadua zitoke kwenu,
Kaburini ni wekeni,Fikirini zamu yenu,
Belgium Udachini, Buriani Ikhiwani.
Wale nilowakosea,Nisameheni Jamani,
Haikuwa yangu nia, Adui yetu Shetani,
Mimi walonikosea, Sina kinyongo Moyoni.
German na Romania,Buriani ikhiwani.
Beti Saba nimefika, Nami nenda Msibani,
Taarifa imefika, Amefariki jirani,
Kifo ninakikumbuka, Na mimi nipo njiani,
Waislamu Wenzanguu, Naaga ningali hai
by;Becker Salim Omar, Master Hassan and Maalim Moussa Kijangwa.

Subscribe to:
Posts (Atom)