Wednesday, December 26, 2012

WAMAREKANI MATARAJIO YA UCHUMIBORA BADO

Karibu asilimia 44 ya Wamarekani hawana matarajio ya kuboreka hali ya uchumi wa nchi hiyo katika kipindi cha mwaka ujao wa 2013. Uchunguzi wa kura ya maoni uliofanywa na gazeti la Kiingereza la Washington Post na kutangazwa leo na kanali ya televisheni ya ABC News unaonyesha kuwa, asilimia 44 ya Wamarekani hawana matarajio ya kuboreka uchumi wa nchi hiyo na kwamba, wananchi hao wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na hali hiyo. Uchunguzi huo wa maoni pia unasisitiza kuwa, zaidi ya theluthi tatu ya watu walioulizwa kuhusiana na jambo hilo wanaamini kwamba, uchumi wa nchi hiyo unaendelea kudhoofika. Serikali ya Rais Barack Obama na Wademocrats nchini Marekani, walikuwa na mazungumzo ya kujadili njia za kuzuia mporomoko wa uchumi, lakini hata hivyo mazungumzo hayo yalimalizika bila kupayikana natija.
Ombaomba wa kimarekani akiwa na bango lake

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO