Wednesday, October 17, 2012

DHUL-HIJJAH

Assalam alaykum warahmatul lahi wabarakatu.Amma baada ya kumshukuru Mwenyezimungu na kumtakia Rehma na Amani Mtume wa Allah na kipenzi chetu mtume Muhammad swallal lahu alayhi wasallam. MSAMU kwa ushirikiano na jumuiya nyingine za kidini inapenda kuwatangazia rasmi kuwa JUMATANO ya Tarehe 17 Oktoba ndio siku ya kwanza ya Dhul- Hijjah na Arafa itakuwa ni siku ya Alkhamis sawa na tarehe 25 Oktoba 2012 na Iydul-Adhw-haa itakuwa ni siku ya Ijumaa tarehe 10 Dhul-Hijjah sawana Oktoba 26.




Pia tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu wengi jambo ambalo wanaghafilika nalo, kuwa, wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa, kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah wanatakiwa wajizuie kukata nywele na kucha mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:


عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إذا رأيتم هلال ذي الحجة وأراد أحدكـم أن يضحّي فليمسك عــن شعره وأظفاره) وفي راوية: ((فلا يأخذ من شعره ولا من أظفـاره حتى يضحّي)) مسلم


Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake)
Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja))[Muslim na wengineo]. 




Siku Kumi Bora Kabisa Za Allah


Inatupasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa neema Aliyotujaalia ya kutuwekea miezi mitukufu, au siku tukufu au nyakati tukufu ambazo vitendo vyake vyema huwa na thawabu nyingi sana. Na hivi tunakaribia kabisa kuingia katika mwezi mwingine mtukufu wa Dhul-Hijjah. Katika mwezi huu, siku kumi za mwanzo ni siku bora kabisa katika dunia na zina fadhila kubwa kutokana na dalili zifuatazo:


عن ابن عباس رضي الله عنهما، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((ما من أيام العمل الصالح فيها أحب إلى الله من هذه الأيام)) - يعني أيام العشر-. قالوا: يا رسول الله، ولا الجهاد في سبيل الله ؟ قال: ((ولا الجهاد في سبيل الله، إلا رجل خرج بنفسه وماله ثم لم يرجع من ذلك بشيء)) البخاري

Imetoka kwa Ibn Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) kwamba Mjumbe wa Allaah amesema: ((Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah kama siku kumi hizi)) (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah) Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo)) [Al-Bukhaariy].


Miongoni mwa ubora wake ni:

1.Amali Zake Ni Bora Kuliko Kwenda Katika Jihaad Fiy SabiliLLaah

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO