Saturday, June 15, 2013

AFRIKA YA KUSINI KUIREJESHEA LIBYA MALI ZA GHADAFI

Afrika Kusini imeafikiana na Libya kurejesha zaidi ya dola bilioni moja zilizokuwa zimefichwa katika nchi hiyo na dikteta Muammar Gaddafi. Pravin Gordhan Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini amesema, uamuzi huo wa kurejeshewa  Libya fedha hizo na mali zilizokuwa za Gaddafi umechukuliwa kwa mujibu wa sheria za Umoja wa Mataifa. Juni 2 magazeti ya Libya yaliandika kuwa, serikali ya Afrika Kusini ilitakiwa kuisaidia kuirejeshea serikali ya Tripoli fedha, dhahabu na almasi za Gaddafi.  Imeelezwa kuwa, baada ya uchunguzi kufanywa ilijulikana juu ya Mali hizo zilizokuwa zimefichwa huko Afrika Kusini na katika nchi nyingine jirani na Gaddafi pamoja na mkuu wa zamani wa vyombo vya ujasusi vya Libya Abdullah al-Senussi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, wananchi wa Libya walianza harakati za kimapinduzi dhidi ya utawala wa karibu miongo minne wa Kanali Muamari Gaddafi Februari 2011 na kufanikiwa kuuangusha utawala huo Agosti 2011 ambapo Gaddafi aliuawa Oktoba 20 mwaka huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO