Mwili wa kiongozi wa zamani wa Palestina, Yasser Arafat, umefukuliwa
kutoka kaburi lake liloko ukingo wa Magharibi mjini Rammala ili kuwawezesha
kuufanyia uchunguzi kubaini iwapo aliuwawa kwa sumu. Bwana
Arafat alifariki dunia mwaka 2004 nchini Ufaransa baada ya kuugua kwa kipindi
kifupi.
Maradhi
yaliyopelekea kifo chake hayakubainika. Uamuzi wa kuufukua mwili wa Yasser
Arafat katika kaburi lake lililoko ukingo wa Magharibi unafuatia makala ya
televisheni iliyodai kupata mabaki ya madini ya kitonoradi aina ya Polonium
kwenye nguo zake.
Wapalestina
wengi wanashuku kwamba huenda Israel ilihusika katika kifo cha kiongozi huyo.
Israel imekuwa ikikanusha shutuma hizo.
Uchunguzi
wa mauaji dhidi ya Bwana Arafat umeanzishwa nchini ufaransa kufuatia ombi
lililowasilishwa na mjane wake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO