Tuesday, January 15, 2013

UTHABITI WA MISRI NI SAWA NA WA GHAZA

Waziri Mkuu wa Serikali Halali ya Palestina iliyochaguliwa kwa njia ya demokrasia amesema kuwa uthabiti wa Misri ni sawa na kuweko uthabiti katika ardhi za Palestina. Ismail Hania amesema kuwa eneo la Ukanda wa Ghaza litalinda na kuunga mkono usalama wa Misri kuanzia mashariki hadi magharibi. Hii ni kwa sababu Wapalestina wanafahamu kuwa uthabiti wa Misri ni sawa na uthabiti wa Ukanda wa Ghaza. Waziri Mkuu wa Serikali Halali ya Palestina pia ameutaja usalama wa mipaka kuwa ni kadhia tukufu na kuongeza kuwa Wapalestina wanataka kurejeshwa amani na utulivu kwenye mipaka ya Misri na kwamba watatekeleza juhudi zao zote katika uwanja huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO